Kwenye
mitandao ya kijamii, wanaharakati kutoka mashirka mbalimbali nchini
Sudan wametoa wito tangu Jumapili Novemba kususia shughuli za serikali
kwa muda wa siku tatu mfululizo.
Wito huu ulitolewa kutokana na uamuzi wa serikali wa kuongeza bei ya mafuta, dawa na umeme.
Hatua hii ya serikali imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali mahitajio.
Raia wa
Sudan wamerusha kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter picha za mitaa
tiliyo upu mjini Khartoum na katika sehemu nyingine za nchi hiyo.
Wakati
huo huo, maafisa wa usalama wa Sudan, mapema Jumatatu hii asubuhi
wamekamata nakala ya magazeti binafsi ya kila siku ya Al-Ayyam na
Al-Jareeda bila maelezo.
Kwa
mujibu wa magazeti yote mawili, kukamatwa kwa nakala hizo inawezekana
kuwa ni adhabu kwa magazeti hayo kutokana na kazi na kuchapishwa kwa
habari hiyo kuhusu wito uliyotolewa na wanaharakati kutoka mashirika
mbalimbali kwa raia kususia shughuli za serikali.
Usalama
wa Sudan inaweka vikwazo vikali kuhusu uhuru wa vyombo vya habari ikiwa
ni pamoja na udhibiti kabla ya kuchapishwa habari yoyote.RFI
No comments:
Post a Comment