Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akiwa
na mgeni wake Ndg Wilfred Moshi wakiwasili katika viwanja vya Baraza la
Wawakilishi Chukwani Zanzibar, kutembelea na kujionea shughuli za
Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Wilfred Moshi ni Mtanzania
wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani wa Evarest ukiwa na Mita 8,848,
Mtanzania huyo Ndg Wilfred Moshi amepanda mlima huo mwaka 2012. akiwa ni
Mwaafrika wa Tatu kupanda mlima huo na mwafrika wa Pili mweusi kupanda
mlima huo Duniani kwa ukubwa.
Ndg
Wilfred Moshi akiwa Zanzibar kwa matembezi na kuangalia Utalii wa
Zanzibar na kupata nafasi kutembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani
Zanzibar kwa mualiko wa Mhe Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar Mhe Simai
Mohammed Said.
Ndg
Wilfred Moshi akitambulishwa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar akiwa Mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai
Mohammed Said (Mpaka Basi) akisalimia Wajumbe wa Baraza wakati wa
kutambulishwa kwake.
Mtanzania
wa Kwanza kupanda Mlima Evarest Ndg Wifred Moshi akiwa katika Ukumbi wa
Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai
Mohammed Said. akiwa katika sehemu ya wageni katika ukumbi huo wa Baraza
Chukwani Zanzibar.
Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akimtambulisha
Mgeni wake Ndg Wilfred Moshi kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe
Zuberi Ali Maulid, alipofika kutembelea na kujionea shughuli za Baraza
la Wawakilishi wakati wa Mkutano wake leo asubuhi.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mtanzania
wa Kwanza na Muafrika wa Tatu Duniani kupanda Mlima wa Evarest Ndg
Wilfred Moshi alipofika katika jengo la Baraza la wawakilishi Zanzibar
akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya
mgeni wake Ndg Wilfred Moshi ambae ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima
Evarest..
Ndg
Wilfred Moshi akitowa historia yake kwa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika katika majengo ya Baraza la
Wawakilishi kwa mualiko wa Mhe. Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Tunguu
Zanzibar. akitowa historia yake ya kufanikiwa kupanda mlima huo mkubwa
duniani na kuelezea tayari ameshapanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara
100.
Ndg Wilfred Moshi akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kumbukumbu yake alipofika kutembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo. 29-11-2016 akiwa mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika picha ya pamoja na Mtanzania wa
Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani wa Evarest Ndg Wilfred Moshi
alipofika katika jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
No comments:
Post a Comment