Mji wa
Santiago unaojulikana kama chimbuko la ukomunisti wa Cuba, ndiko
mapinduzi yaliyoongozwa na marehemu Castro yalianzia mnamo mwaka 1953 na
akachukua urais mwaka 1959.
Baada ya
mamia ya maelfu ya watu kuhudhuria misa ya wafu kwa mwanamapinduzi wa
Cuba Fidel Castro, majivu ya marehemu huyo yanaanza kusafirishwa leo
kutoka jiji kuu Havana hadi Santiago kufanyiwa mazishi hapo siku ya
Jumapili. Huo ukiwa umbali wa kilomita 900. Maelfu kwa maelfu ya wacuba
wanatarajiwa kuwa barabarani kushuhudia majivu hayo yatakapokuwa
yakisafirishwa.
Mwili wa
Fidel Castro aliyefariki akiwa na umri wa miaka 90, Ijumaa wiki jana,
ulichomwa moto kulingana na matakwa yake. Majivu yake yatapitishwa
katika miji kadhaa nchini humo kwa siku tatu kwanzia leo, kabla ya
kufikishwa mji wa Santiago ambako ndiko atazikwa siku ya Jumapili.
Mji wa
Santiago unaojulikana kama chimbuko la ukomunisti wa Cuba, ndiko
mapinduzi yaliyoongozwa na marehemu Castro yalianzia mnamo mwaka 1953 na
akachukua urais mwaka 1959. Hapo jana mamia ya maelfu ya waombolezaji
walifika kumpa heshima za mwisho jijini Havana.
Rais wa
Bolivia ni miongoni mwa waliohudhuria misa hiyo na alisema: "Fidel
hajafa kwa sababu wanaopigania uhuru hawafariki. Huyo ni Fidel. Hajafa
kwa kuwa mawazo hayafi hasa mawazo yanayoleta ukombozi. Fidel hajafa kwa
kuwa mapigano hayajaisha hasa mapigano dhidi ya utengano. Fidel ni kama
yuko hai kuliko zamani akiendeleza vita kuokoa makazi yetu ya pamoja".
Mazishi
yake yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa
wakiwemo marais Nicolas Maduro wa Venezuela, Daniel Ortega wa Nicaragua,
Evo Morales wa Bolivia na Rafael Correa wa Equador, kando na wakuu wa
nchi za Amerika ya kusini na mfalme wa zamani wa Uhispania Juan Carlos.
Uhusiano wa Cuba na Marekani
Fidel
Castro alitawala Cuba kwa miaka 47, hadi alipojiuzulu mwaka 2006
kufuatia hali yake ya kiafya, na kumkabidhi nduguye Raul Castro. Tangu
wakati huo hajajitokeza hadharani japo inaaminika alikuwa na wasiwasi na
uhusiano ulioimarishwa mwaka 2014 kati ya nchi yake na hasimu wao wa
jadi Marekani. Haijabainika ikiwa uhusiano huo utaendelea kuimarika
baada ya Januari rais mteule wa Marekani Donald Trump atakapochukua
rasmi urais.
Akitoa
hotuba ya rambirambi jijini Havana, rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
amesema "Cuba haikutafuta madini ya dhahabu, almasi au mafuta barani
Afrika. Wacuba walitaka uhuru na mwisho wa unyanyasaji wa bara la Afrika
kutumiwa kama kiwanja cha kuchezewa na nchi kubwakubwa huku watu
wakiteseka".
Fidel
Castro alipendwa na wengi duniani hasa Amerika ya kusini na Afrika, kwa
kusimama dhidi ya Marekani, huku akizindua mipango ya elimu bure na
huduma za afya bila malipo kando na kuwatuma madakitari wao katika
mataifa mengine duniani kutoa misaada ya kiafya.
Lakini
wengine walimshutumu kuwa kiongozi wa kiimla aliyevuruga uchumi kutokana
na sera zake za usosholisti na kuwanyima wacuba haki za kibinadamu
mfano uhuru wa kujieleza.DW
No comments:
Post a Comment