Rais wa
Nogeria, Muhammadu Buhari asema kusononeshwa na ripoti ya Humana right
Watch kuhusu tuhuma za ubakaji zinazowakabili askari wake.
Rais wa
Nigeria ameamuru uchunguzi kuhusu madai ya unyanyasaji wa kijinsia
katika makambi yaliyojengwa kwa minajili ya kuwapokea watu waliokimbia
machafuko yaliyokuwa yakitekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la
Boko Haram.
Kwa
mujibu wa Ofisi ya rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari "alishtushwa" na
ripoti ya shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch
(HRW) ambalo linawashtumu maafisa wa vikosi vya usalama vya nchi yake
kuwabaka wanawake katika makambi hayo ya wakimbizi.
Rais
Muhammadu Buhari ameitaka polisi na Wakuu wa majimbo husika kuanza mara
moja uchunguzi ili kutoa mwanga juu ya madai ya HRW.
Kwa mujibu wa Human Right Watch, wanawake 43 walibakwa au kutumiwa kingono na maafisa wa usalama na makundi ya wanamgambo.
Vitendo
hivi vya ubakaji vilifanyika katika makambi yaliyojengwa hasa katika
jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi, kwa minajili ya kuwapokea
watu waliolazimika kukimbia mauaji yaliyokua yakitekelezwa na wanamgambo
wa Boko Haram.
Baadhi ya
wanawake waliokuwa wakiishi katika makambi wamesema walilazimishwa
kufanya ngono na kutelekezwa wakati walipata ujauzito, kwa mujibu wa
Human Rights Watch.
Machafuko
yanayoendeshwa na kundi la kijihadi nchini Nigeria yamesababisha maelfu
ya watu kupoteza maisha na watu zaidi ya milioni mbili wamelazimika
kuyahama makazi yao.
RFI
No comments:
Post a Comment