Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ,Hamad Masauni, akikata utepe kuashira ufunguzi
wa kituo kipya cha kisasa cha huduma ya magari madogo na makubwa
kilichopo Magomeni Mwembe chai jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, Kushoto
ni Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani ,Mohamed Mpinga na Meneja
usambazaji kanda ya Afrika Mashariki Dkt.Fulgence Bube.
Mkurugenzi
mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, akimsikiliza kwa
makini,Naibu waziri wa mambo ya Ndani ,Mhandisi Hamad Masauni katika
hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha kutoa huduma kwa magari makubwa na
madogo kilichopo Magomeni Mwembe Chai jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, akizungumza na
wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo kipya cha huduma kwa wateja.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mhandis Hamad Masauni, akizungumza na wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo cha wateja.
Wadau wa mbalimbali wakifuatilia uzinduzi.
Msimamizi wa kituo cha kutoa huduma za magari cha Mwembechai akitoa maelezo kwa waziri na viongzi mbalimbali.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Superdoll wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa
uzinduzi wa kituo cha kisasa cha kutoa huduma ya magari makubwa na
madogo kilichopo Magomeni mwembe chai jijini Dar es Salaam.
Watanzania
wanaotumia vyombo vya moto wametakiwa kufanya uchunguzi wa mara kwa
mara kabla ya kuanza safari ili kuweza kupunguza ajali za barabarani.
Hayo
ameyasema Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Ahamad Masauni wakati wa
uzinduzi wa Kituo cha Kisasa cha kutoa huduma ya magari makubwa na
madogo, amesema kuwa kufanya uchunguzi wa magari katika kituo hicho
kitasaidia kupunguza ajali barabarani.
Amesema
teknolojia inakua kwa kasi hivyo magari ya sasa yanatakiwa kufanyiwa
uchunguzi wa kisasa kabla ya kuanza kwa safari katika kituo cha mwembe
chai.
Masauni
amesema Superdoll wamekuwa wabunifu wa teknolojia ya kisasa ya katika
vyombo vya moto ikiwa ni kuweka safari kuwa salama kwa safari zote.
Amesema
kuwa kunzisha kituo hicho watakuwa wamesaidia ujenzi katika masuala ya
usalama barabani na kuweza kupunguza ajali za barabarani.
Masauni
amesema kuwa watashirikiana na superdoll na kampuni ya matairi ya
Michelin katika kufanya uchunguzi wa magari kwa teknolojia ya kisasa
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabani, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi,
Ahmed Mpinga amesema superdoll wamekuwa wadau wa usalama barabarani na
kuendelea kuwa wabunifu katika teknolojia mbalimbali.
Amesema
wanaomiliki vyombo vya moto watumie kituo cha uchunguzi wa teknolojia ya
katika kuweza usalama wa gari na maisha watu katika kufikia lengo la
serikali ya kupunguza ajali barabarani.
No comments:
Post a Comment