Katibu tawala wilaya ya Chemba,Ndugu Nyakia Ally
Katika
kuadhimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwl
Julius Kambarage Nyerere, Maadhimisho ya kilele cha wiki ya Vijana
pamoja na Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru hapo kesho tarehe
14/10/2016.
Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Ndugu Nyakia Ally,alipokuwa akizungumza na Globu ya Jamii kwa njia ya Simu,leo.
Nyakia amesema kuwa Wilaya ya Chemba imepanga kufanya yafuatayo katika kuenzi harakati na juhudi za Muasisi huyu wa Taifa letu.
Ikumbukwe
Mwl Nyerere katika maisha yake alipigania ukombozi wa Tanzania katika
1. Kupambana na adui ujinga. 2. Adui Maradhi. 3. Adui Umasikini na 4.
Adui njaa.
"Hivyo
Wilaya yetu itaadhimisha siku hii kwa kushiriki kwa kusafisha eneo
itakapojengwa Zahanati ya Wilaya ya Chemba na wananchi watachangia
matofali ya ujenzi wa Zahanati hiyo. Vile vile zoezi hilo litaendana na
uchangiaji wa damu katika benki ya damu hapa Wilayani Chemba",alisema
Nyakia
Amesema
kuwa baada ya kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kijamii,baadae
Kutakuwepo na Michezo mbalimbali ya kuvuta kamba baina ya Watumishi wa
Serikali na Wananchi wa Kijiji cha Chemba,Kukimbiza kuku na mwisho
kutakuwa na mchezo wa bao kati ya Wazee wa hapa Chemba katika kumuenzi
Mwl Nyerere ambaye alikuwa mpenzi mkubwa wa mchezo huu.
Amesema
kuwa Washindi katika mchezo wa kuvuta kamba na nao watajinyakulia zawadi
ya Mbuzi na ule wa kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake na wanaume
watajinyakulia kuku watakaye mkamata.
No comments:
Post a Comment