Tarehe
12.10.2016 majira ya saa 16:35 katika eneo la Busenga “A” kata ya
Buswelu wilaya ya Ilemela jiji na mkoa wa Mwanza, askari walifanikiwa
kumkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Juma Biria miaka 42,
mfanya biashara na mkazi wa mtaa wa Busenga akiwa na vifaa vya
kutengeneza noti bandia ambavyo ni kemikali ikiwa ndani chupa kubwa,
sabuni ya maji iliyowekwa ndani ya chupa ndogo, karatasi zilizokatwa
mfano wa noti ya shilingi elfu kumi pamoja na unga ambao bado
haujafahamika ni wa kitu gani, kitendo ambacho ni kinyume na sheria na
taratibu za nchi .
Inadaiwa
kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu akishirikiana na wenzake amekuwa akifanya
shughuli hiyo ya uhalifu, ndipo zilipatikana taarifa za kiintelejensia
kuhusiana na uhalifu huo, ndipo askari waliweza kufuatilia na kufanikiwa
kumtia nguvuni mtuhumiwa huyo.
Aidha
kwa sasa jeshi la polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa, pindi
uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki za
kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake. Aidha jitihada za kuwasaka
wenzake wanaodaiwa kushirikiana na mtuhumiwa huyu katika uhalifu huo
bado zinaendelea.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa
rai kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza, akiwataka kushirikiana na
jeshi la polisi katika kupambana na wahalifu wa aina kama hii, ili
waweze kufikshwa katika vyombo vya sheria, kwani jeshi la polisi
linaamini endapo wananchi wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lao,
tutaweza kukomesha uhalifu katika mkoa wetu.
imetolewa na:
DCP: Ahmed Msangi
Kamanda wa polisi (m) Mwanza
No comments:
Post a Comment