Mwenyekiti
wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza na wanachama wa mtandao huo
wakati wa mkutano wa kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi, Kagera.Picha
na Mpiga picha wetu.
Mwanachama
wa SHIWATA, Hamisi Kiondo akichangia hoja ya namna ya kusaidia
waliopatwa na maafa Kagera. (Picha na Mpiga Picha Wetu).
Na wandishi Wetu
Mtandao
wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unatarajia kukabidhi mchango wa maafa ya
tetemeko la ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera baada ya siku ya awali
iliyokuwa imepangwa ya Oktoba 14, 2016 ya maadhimisho ya kumbukumbu ya
kfo cha Mwalimu Nyerere kuingiliana na ratiba nyingine za kitaifa.
Mwenyekiti
wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza katika mkutano wa wanachama jana
alisema mpaka sasa fedha ambazo zinatarajiwa kukabidhiwa ni sh. 600,000
ambazo kati ya hizo 100,000 zimechangwa na wanachama katika mkutano huo.
Alisema
wakati maandalizi ya kukabidhi fedha hizo ukiendelea siku hiyo ambayo
SHIWATA imetenga kwa ajili ya kufanya kazi za kumuenzi baba wa Taifa,
Nyerere viongozi wa kitaifa ambao walikuwa wapokee mchango huo watakuwa
mkoa wa Simiyu katika sherehe ya kuzima Mwenge wa Uhuru.
Katika
mkutano huo wanachama waliahidi kuendelea kuchangia matukio yote ya
kijamii na wengi wameahidi kuwasilisha vifaa mbalimbali na nguo kwa
waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.
Wakati
huo huo SHIWATA imetoa ofa ya Sh. Mil. 3.2 kwa wanachama wake
watakaojenga nyumba za kuishi katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga.
Akifafanua
kuhusu ofa hiyo, Taalib alisema gharama za kusafirisha vifaa vya
ujenzi, gharama za kusafisha eneo la kujenga na ekari moja ya kulima
bustani watapewa bure.
Alisema
kasi ya wanachama kujenga na kuhamia kijijini inaridhisha mpaka sasa
nyumba 200 zimekamilika na nyingine zinaendelea kujengwa.
No comments:
Post a Comment