Kufuatia
ripoti za matukio mengi ya watumiaji wa simu za Samsung kulipukiwa na
simu hizo wakati wa kuchaji, kampuni hiyo ya Kikorea hatimaye imewataka
watumiaje wake kutupa toleo la ‘Galaxy Note 7’ kutokana na tatizo hilo.
Kampuni
ya Samsung imetoa tamko rasmi kupitia tovuti yake ikiwataka watumiaji
wa simu hizo toleo la ‘Galaxy Note 7’ duniani kote kuchukua tahadhari na
kuacha kabisa kuzitumia wakati ikiendelea na uchunguzi zaidi.
“Tunafanya
kazi na Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusu kuwepo kwa ripoti za
matukio yanayohusu Galaxy Note7. Kwa sabababu usalama wa mteja wetu ni
kipaumbele, Samsung tunawataka wauzaji wote wa simu zetu duniani kuacha
mara moja kuuza Galaxy Note 7,” imeeleza taarifa rasmi ya kampuni hiyo.
Majaribio
ya betri ya simu ya Samsung, Galaxy Note 7 yaliyofanywa katika maabara
moja nchini Singapore yalipelekea simu hiyo kulipuka moto.
Hivi
karibuni, hata hapa Tanzania, kumekuwa na ripoti za matukio ya wananchi
wengi kudai kuwa wameripukiwa na simu za Sumsung walipokuwa wanachaji.
Pia,
kulikuwa na taarifa ambazo hazikuthitishwa na Mamlaka kuhusu watu
kulipukiwa na simu hizo walipozipokea wakati zikiwa kwenye chaji.
No comments:
Post a Comment