Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange jana
tarehe 05 Oktoba, 2016 amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu
hapa nchini na kurejea nchini kwake.Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Rais Kabila aliagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Viongozi wengine walioungana na Rais Magufuli wakati wa kumuaga Rais Kabila ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda na Viongozi wa Dini.
Katika hatua nyingine, mara baada ya kuondoka kwa Rais Kabila, Rais Magufuli alifanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.
Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.
Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili waliotoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.
"Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua" alisisitiza Dkt. Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mara baada
ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kurejea DRC.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipunga mkono kuagana na
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila (hayupo pichani)
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Makamu wa Rais Samia Suluhu akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika
uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One kuangalia
ufanisi wa mashine hizo.
No comments:
Post a Comment