Mkemia
Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele (kulia), akitoa hotuba wakati
wa hafla ya utoaji zawadi kwa wanafunzi na walimu Bora wa masomo ya
Kemia na Baiolojia kwa kidato cha Nne na kidato Tano 2014/2015
iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Mgeni
Rasmi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Michael John (kulia)
akitoa hotuba kabla ya kukabidhi zawadi kwa Wanafunzi na Walimu Bora wa
masomo ya Kemia kwa Kidato cha Nne waliomaliza mwaka 2014 na cha Sita
2015. Jumla ya wanafunzi Ishirini na Nne (24) na walimu wane (4)
walifanikiwa kupewa zawadi kwenye hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya
Ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali, Jijini Dar es Salaam.
Mhariri
Mtendaji wa Magazeti ya Serikali, Dkt. Jim Yonazi (kulia) akitoa neno la
shukrani kwa niaba ya wazazi wa wanafunzi waliopata zawadi kwa kufanya
vizuri kwenye masomo ya Kemia na Baiolojia kwa Kidato cha Nne 2014 na
Kidato cha Tano 2015. Dkt Yonazi alimsindikiza kijana wake Yonazi
Charles Senkondo kwenye hafla hiyo
Mwanafunzi
Bora wa masomo ya Kemia na Baiolojia kwa upande wa wasichana wa kidato
cha sita mwaka 2015, Meghna Solanki (kulia) akitoa neno la shukrani kwa
niaba ya wanafunzi wenzake baada ya kupatiwa zawadi zao.
Wanafunzi
Bora wa masomo ya Kemia na Baiolojia kwa Kidato cha Nne na Tano kwa
mwaka 2014/2015 wakitambulishwa wakati wa hafla ya kuwapa zawadi
iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
Rasmi, Bw. Michael John, akimkabidhi zawadi mwanafunzi, Yonazi Charles
Senkondo (kulia) baada ya kuwa mwanafunzi bora kwenye masomo mawili ya
Kemia na Baiolojia kwa kidato cha Sita mwaka 2015.
Mgeni
Rasmi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Michael John (wa pili
kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za
Vinasaba vya Binadamu, Bi. Gloria Omari (kushoto) akieleza shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Idara hiyo. Wengine kutoka kulia ni Mjumbe wa
Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,
Profesa Esther Lugwisha na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel
Manyele (wa tatu kulia). Mgeni Rasmi alikuwa akimuwakilisha Naibu
Waziri, Mhe. Hamisi Kigwangalla kwenye Tuzo kwa wanafunzi na walimu Bora
wa masomo ya Kemia na Baiolojia kwa Kidato cha Nne 2014 na cha Sita
2015.
Mgeni Rasmi, Bw. Michael John (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala, Profesa Esther Lugwisha (wa pili kushoto), Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele (wa pili kulia), Menejimenti ya Wakala, wageni waalikwa, walimu na wanafunzi mara baada ya kumaliza zoezi la utoaji zawadi kwa wanafunzi na walimu Bora wa somo la Kemia na Baiolojia kwa Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Sita 2015
No comments:
Post a Comment