Friday, October 21, 2016

Neno La Leo: Tusigombane Wenyewe Mbele Ya Wahisani..


Ndugu zangu,

Tumeshuhudia biashara ya aibu tukiianika mbele ya macho ya walimwengu.

Tulichokiona kule Arusha kinatufedhesha kama taifa. Tunajenga nyumba moja na hatupaswi kugombania fito.

Mtanzania Shaaban Robert aliandika miaka 80 iliyopita; "Kama Ulaya, Kama Afrika...!"

Ndio, mwandishi Shaaban Robert alipata kuandika waraka wa gazetini wenye kichwa hicho cha habari. ( Gazeti Mambo Leo, Juni, 1932).

Shaaban Robert anaandika; ” Nina hakika ya kuwa labda baada ya miaka mingi watakaoturithi wataweza kusema Kama Ulaya, Kama Afrika!

Bara kubwa maskini lililokuwa katika giza kwa muda mrefu , hata Wazungu walipofika watu walikuwa wakitiana vidole machoni mchana, kila mahali palikuwa na soko la biashara ya aibu. Sasa, taa ya ustaarabu yawaka na nuru yake yaangaza” - Shaaban Robert.

Hapana Shaaban Robert, huko ulikolala na ujue, kuwa soko la biashara ya aibu linaendelea na linazidi kupanuka. Ndio, ni aibu, kwamba tunashindwa kuyamaliza mambo yetu kwa mazungumzo ya kistaarabu na zaidi kuweka misingi ya kuondokana na mambo haya ya hovyo hovyo, tena mbele ya wahisani.

Na kwa mtazamo wangu, kinachotutesa na kutuletea aibu ni kuendekeza ya Uvyama, badala ya Utaifa; UCcm, UChadema na UCuf, badala ya Utanzania.
Shame on us.
Maggid,

No comments:

Post a Comment