Na Mahmoud Ahmad Longido
Mkurugenzi
halmashauri ya Longido bwana Juma Mohamed Muhina ameamuru kukamatwa na
kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi mtendaji wa kata ya Egirai Lumbwa
Wilayani Londigo bwana Paulo Luka kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za
ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Natroni Flamingo.
Maamuzi
hayo yamefikiwa baada ya wananchi wa kijiji cha Meligoi kata ya Egirai
Lumbwa kuikata taarifa iliyosomwa na mtendaji wa kata hiyo iliyoonyesha
ujenzi mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha milioni 50 lakini michango
ya awali ilikuwa milioni 12 na kati ya hiyo milioni 4 tu ndio ilikuwa
michango ya wananchi.
Wananchi
hao walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa
akisikiliza Changamoto mbalimbali walizonazo baada yakufanya ziara
katika kijiji hicho , walisema kuwa wao wanavyojua wamechanga zaidi ya
fedha zilizotajwa kwenye taarifa hiyo.
Hivyo
Gambo alimtaka Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri kufafanua juu ya matumizi
ya fedha hizo, akifafanua Bi. Mwajuma mdaira alisema alifanya ukaguzi
na kugundua kuwa fedha zilizokusanywa kwa njia ya michango ilikuwa
milioni 95 na milioni 50 kati ya hizo zilitumika kwenye marekebisho ya
majengo ya shule japo hakukuwa na mikata yoyote iliyoingiwa kati ya
shule na mkandarasi.
Pia fedha
hizo zilitumika bila kutumia stakabadhi za malipo za halmashauri, na
kuna wawekezaji 2 ambao ni Winget Windros Safari walichangia mifuko 200
ya simenti na mingine 200 ilitolewa na Kilomberong Hunting kusaidia
ujenzi lakini mifuko 144 kati ya hiyo iliuzwa na fedha zake hazikujulika
matumizi yake lakini bado anaendelea na ukaguzi zaidi.
Hivyo
kumpelekea Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kutaka kufahamu hatma ya mtendaji
huyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri aliyekili kupata taarifa hiyo jana
yake tu na hapo hapo akamuamuru kamanda wa polisi Wilaya kumkamata
mtendaji huyo nakumpeleka kituoni kwa maelezo na upelelezi zaidi juu ya
ubadhilifu huo.
No comments:
Post a Comment