Wanamuziki
wa bendi ya Msondo Ngoma Shaban Dede kulia na Hassan Moshi wakiimba
jukwaani katika moja ya maonesho ya bendi hiyo jijini Dar es salaam.
Katibu wa kamati ya maandalizi ya Maonyesho hayo ya kila mwezi Bw.Abdulfareed Hussein
Bendi
kongwe ya muziki wa dansi nchini,MSONDO NGOMA MUSIC BAND(BABA YA
MUZIKI),inakuletea onyesho lao kubwa la kila mwezi maalum kwa
wanafamilia wa Msondo Ngoma na wadau wa muziki wa dansi maarufu kwa jina
la MSONDO NGOMA FAMILY DAY,ambalo kwa mwezi huu litafanyika wilaya ya
Ilala katika ukumbi wa Lekham Hotel,Buguruni.
Akiongea
na fullshangwe blog,Seneta wa Bendi hiyo ambaye pia ni katibu wa kamati
ya maandalizi ya Maonyesho hayo ya kila mwezi Bw.Abdulfareed
Hussein,ameeleza kwamba baada ya mafanikio makubwa katika maonyesho
yalopita,sasa burudani itaangushwa Lekham Hotel,ikiwa na kauli mbiu ya
CHANGIA BENDI YAKO,CHANGIA BIMA YA AFYA KWA WANAMUZIKI WETU.
Katibu
huyo pia amefafanua kwamba onyesho la mwezi huu litakuwa maalum la
kuchangia upatikanaji wa bima ya afya kwa wanamuziki wa Msondo ngoma.
Bendi
hiyo imedhamiria kuja na mipango mbalimbali katika kuendeleza muziki wa
dansi na kadri siku zinavyokwenda ndivyo mikakati mbalimbali
itakavyotekelezwa.
Katika
onesho hilo pia kutakuwa na zawadi kwa mtu atakayecheza vizuri mtindo wa
msondo ngoma , atakayeimba vizuri nyimbo ya mashindano ya Msondo Ngoma
na atakayependeza zadi katika siku hiyo.
Kiingilio
katika onyesho hilo kitakuwa ni 10,000,japo wadau wanaruhusiwa
kuchangia zaidi ya bei hiyo na kwa mawasiliano ya uchangiaji wa awali
unaweza kumpata na kukupa maekekezo kupitia namba ya simu 0653909050.
No comments:
Post a Comment