Maafisa
wanataka majibu baada mshukiwa wa ugaidi kujiua gerezani. Jaber Albakr
alipatikana akiwa amejinyonga katika chumba cha gereza alilokuwa
akizuiliwa katika mji wa Leipzig.
Waziri wa
usalama wa ndani Thomas de Maziere amesema kifo cha Albakr huenda
kikavuruga juhudi za kuwasaka washirika wake. Wakili wa Al Bakr
Alexander Huebner mwanasheria wa mji wa Dresden, ameliambia gazeti la
Focus kuwa gereza la Leipzig lilikuwa linafahamu kuwa mteja wake alikuwa
katika hatari ya kujiua baada ya kuonyesha dalili hizo.
Mkimbizi
huyo kutoka Syria alijiua jana usiku,siku mbili baada ya kutiwa
mbaroni.Vyombo vya habari hapa ujerumani viliripoti kuwa mtuhumiwa huyo
alifanikiwa kujinyonga japo msemaji wa wizara ya sheria katika jimbo la
Saxony Joerg Heroid hakuthibitisha taarifa hiyo au kutoa maelezo
zaidi.Mamlaka katika jimbo hilo ilikuwa tayari inakosolewa, baada ya
mshukiwa huyo raia wa Syria kufanikiwa kuwakwepa polisi siku ya jumamosi
walipokuwa wakijitayarisha kuvamia ghorofa alilokuwa akiishi katika mji
wa Chemnitz. Ndani ya chumba alichokuwa akiishi polisi walikuta bomu la
uzito wa gramu 1.5 na alikuwa akitumia mtandao kupata maelekezo ya
kutengengeza bomu hilo.
Jemgo alikokamatwa Jaber Albakr
Jaber Albakr hakuonyesha dalili zozote za kuwa hatari
Albakr,
ambaye alikuwa amepewa hifadhi baada ya kuingia Ujerumani mwaka uliopita
hatimae alitiwa mbaroni jumatatu wiki hii eneo la Leipiz baada ya raia
wengine wa Syria wanaoishi eneo hilo kumfunga kwa kamba na kisha
kuwaarifu polisi. Mshukiwa huyo alipewa hifadhi baada ya kuwasili nchini
Ujerumani mwaka uliopita na alikuwa akifwatiliwa na wapepelezi tangu
mwezi uliopita.Hapo jana waziri wa uslama wa ndani De maziere alisema
raia huyo wa Syria alikuwa ameshachunguzwa na kuthibitika kwamba
hakuonyesha dalili zozote za kugeuka na kuwa hatari. Maofisa Ujerumani
waasema inaaminika mshukiwa huyo alikuwa na ushirikiano na kundi
linalojiita dola la Kiislamu IS , na walidhani alikuwa anapanga
kuushambulia uwanja wa ndege wa Berlin wiki hii.
Uwanja wa ndege wa Schönefeld Berlin
Raia
watatu wa Syria waliomtia mbaroni Jaber Albakr w amepewa rasmi uhamisho
na waziri de Maizere alisema wanahitaji pongezi na kutambuliwa kutokana
na ujasiri wao.Polisi bado wanamzuiliwa mtuhumiwa mwingine anayeshukiwa
kupanga shambulizi hilo la bomu lilotibuliwa ambae jina lake
limetambulishwa tu kama Khalil A kuambatana na sheria za Ujerumani za
kutofichua siri ya mtu binafsi. Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 33
raia wa Syria alikuwa akiishi ghorofa la Chemnitz ambako polisi walikuta
bomu hilo .DW
No comments:
Post a Comment