Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akipokea zawadi ya
kitabu kinachoelezea njia zilizotumiwa na nchi ya Korea Kusini, kupiha
hatua kubwa ya maendeleo, kutoka kwa Afisa Mikopo wa Benki ya Exim ya
Korea Kusini, Park Gil Jong, kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa
tano wa ushirikiano wa Korea Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini
Seoul, Korea Kusini.(Picha zote na Benny Mwaipaja-WFM (Wizara ya Fedha
na Mipango)
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akionesha kitabu
alichozawadiwa na kuelezea umuhimu wake kwa nchi za Kiafrika kukisoma na
kukielewa kitabu hicho ili ziweze kuiga mbinu ambazo nchi hiyo
imezitumia hadi kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kiuchumi duniani.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (Katikati) akiwa na ujumbe
wa maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango makao makuu, TRA Tanzania
Bara na Zanzibar, Ofisi ya Mwanasheri Mkuu wa Serikali, wanaoshiriki
kujadili mkataba wa kuepusha kutoza kodi mara mbili kwa raia wa nchi
mbili za Tanzania na Korea, wakiwa mjini Seoul, Korea Kusini.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwasili kwenye ukumbi wa
mikutano wa Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea kwaajili ya
ufunguzi wa mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea
Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEK), Mjini Seoul, Korea Kusini.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akibadilishana mawazo na
maafisa kutoka Tanzania kabla ya kuanza kwa mkutano wa Tano wa
Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Kiafrika(
KOAFEC), uliofanyika mjini Seoul Korea Kusini. Katikati ni Mkuu wa idara
ya kutafuta rasilimali kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Sabra
Issa Machamo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Decklan Mhaiki.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akibadilishana mawazo na
watendaji wakuu wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini Kabla ya kufunguliwa
Rasmi kwa Mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea
Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), unaofanyika Mjini Seoul, Korea
Kusini.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa katika picha ya
pamoja na wapili kushoto, akiwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni
Waziri wa Fedha wa Korea Kusini, Yoo II Ho (kushoto kwake) na Rais wa
Benki ya EXIM-Korea, Lee Duk-Hoon (Kulia kwa Waziri), kabla ya kuanza
rasmi kwa Mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea
Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), katika ukumbi wa Grand
Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini.
Mawaziri
wa Fedha kutoka nchi 54 za kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Tano wa
ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi Afrika (KOAFEC)
wakiweka alama ya kiganja cha mkono kwenye kibao chenye malighafi
maalumu yanayoshika alama za vidole kuonesha ushirikiano na umoja, baada
ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo katika ukumbi wa Grand
Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa ameshika kibao
alichoweka alama ya kiganja chake, kuunga mkono umoja na mshikamano wa
nchi za Kiafrika zinazohusiana kiuchumi na Korea Kusini baada ya
kufunguliwa kwa mkutano wa Tano wa ushirikiano huo kati ya Korea Kusini
na nchi za Afrika (KOAFEC) katika ukumbi wa Grand Intercontinental,
Seoul Parnas, Korea Kusini.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (Katikati) (Kulia
kwake) na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Akinwumi Adesina,
(Kushoto) Baada ya kufunguliwa Rasmi kwa Mkutano wa Tano wa Ushirikiano
wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Kiafrika, unaofanyika Mjini
Seoul, Korea Kusini
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa na Maafisa kutoka Tanzania, wakitoka kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini, baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika, mjini Seoul, Korea.
No comments:
Post a Comment