Sunday, October 9, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MEATU

o1
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt  Seif Shekalaghe kushoto akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu Kulia  Mhe. Elieza Chilagali katika kata ya  Kobondo wilayani Meatu mkoani Simiyu mwishoni mwa wiki.
o2
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (MB) wa Kisesa akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkimbiza mwenge kitaifa kutoka kwa Bw. James Sadick Munguji kutoka Simiyu, katika Mbio za Mwenge Wilayani Meatu mwishoni mwa wiki.
o3
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina  (kushoto) kulia ni kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bw. George Jackson Mbijima na wajumbe wengine wakimsikiliza Bi Regina Anthon katikati alikyeshika kipaza sauti ambaeni ni katibu wa kikundi cha lishe cha mshikamao wilayani Meatu, wakati wa maonyesho ya shughuli za kikundi hicho baadaya kuupokea Mwenge wa Uhuru katika mji mdogo wa Mwandoya jimboni Kisesa.
o4
Katika Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kushoto kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Bw. George Jackson Mbijima na wajumbe wengine pichani wakisikiliza ripoti ya nidhamu katika Eneo la Nyakanja jimboni Kisesa Wilayani wakati wa Mbio za mwenge mwishoni mwa Wiki. (Picha zote na Evelyn Mkokoi Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment