Makamu wa mwenyekiti wa CCM Tanzania bara ,Philip Mangula akiweka
shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa
wa Iringa marehemu Tasili Mgoda wakati wa mazishi yaliyofanyika juzi
mjini Mafinga
Waziri
wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge
wa jimbo la Isimani mkoani Iringa akiweka shada la maua katika kaburi
la aliyekuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Iringa marehemu Tasili
Mgoda wakati wa mazishi yaliyofanyika juzi mjini Mafinga
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini mahamudu Mgimwa (kushoto ) na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto wakiweka shada
la maua katika kaburi la aliyekuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa
Iringa marehemu Tasili Mgoda wakati wa mazishi yaliyofanyika juzi mjini
Mafinga
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini akiweka
shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa
wa Iringa marehemu Tasili Mgoda wakati wa mazishi yaliyofanyika juzi
mjini Mafinga
Mwakilishi wa vyama vya upinzani kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Mufindi akiweka shada
la maua katika kaburi la aliyekuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa
Iringa marehemu Tasili Mgoda wakati wa mazishi yaliyofanyika juzi mjini
Mafinga
MAKAMU
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Philip
Mangula ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Iringa na mikoa ya
jirani katika mazishi ya aliyekuwa mwasisi wa TANU na mwenyekiti
mstaafu wa CCM mkoa wa Iringa Tasili Mgoda aliyefariki Oktoba 14
wakati wa kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu
Julius Nyerere na kuzikwa jana katika makaburi ya Mafinga wilaya ya
Mufindi.
Mangula
katika salamu zake alisema kuwa siku mbili kabla ya kifo chake
Mgoda alimpigia simu japo kwa bahati mbaya hakuweza kuwasiliana
kutokana na kuwa katika mkutano na kuwa kati ya watu na viongozi
ambao walikuwa na upendo kwa wengine marehemu Mgoda ni mmoja na hivyo
kuwataka wanafamilia ,wananchi wa Mufindi na wana CCM kudumisha
upendo na kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu zaidi kama njia ya
kumuenzi marehemu huyo na baba wa Taifa ambao katika uongozi
wao waliweza kuongoza kwa kuzingatia misingi ya uadilifu .
Alisema
kuwa Mgoda kuna mambo mengi ambayo hayaelezeki aliyoacha kama
kielelezo cha uzalendo wake ndani ya wilaya ya Mufindi ambako
alianzisha shule za shirika la elimu Mufindi ( MET) lakini katika
Taifa ni moja kati ya watu waliofanya kazi kwa karibu na mwalimu
Nyerere ila katika ukombozi wa Taifa la Namibia kwa kumhifadhi
mpigania uhuru wa Namibia Rais wa Kwanza wa nchi hiyo Sam Nujoma
akiwa anafukuzwa na serikali ya wakoloni nchini mwake .
Alisema
kuwa marehemu Mgoda alikuwa ni mtu mwenye upendo kwa wote na
hakupenda makuu katika utawala wake hivyo ni vizuri kuendelea
kumuenzi kwa kutenda mema na kupendana zaidi.
Mwenyekiti
wa UWT Mufindi Marcelina Mkini alisema kuwa wao kama wanawake
wanatambua mchango mkubwa ambao Mgoda aliutoa kwao ikiwa ni pamoja na
kujenga misingi bora ya uongozi ndani ya chama na jumuiya hiyo na
kuwa katika wilaya ya Mufindi ni mengi ambayo ameyafanya na kubwa
zaidi ni kupigania uanzishwaji wa mji mdogo wa Mafinga na barabara ya
lami kutoka Mafinga kwenda Madibila wilaya ya Mbarali .
Alisema
kuwa yote hayo ameyafanya wakati akiwa mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Mufindi na kubwa zaidi ni uongozi wake uliotukuka kwa
kuongoza chama kama mwenyekiti kwa miaka zaidi ya 40 katika maeneo
mbali mbali .
Marehemu
akiwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa aliweza kupigania ujenzi wa
barabara ya Lami kutoka Iringa – Dodoma na baada ya kukamilika kwa
ujenzi huo alifurahi zaidi na kuwa sasa yupo tayari kufa wakati
wowote kwani furaha yake imetimia .
”
Enzi ya uhai wake alitupa moyo sana wanawake wa wilaya ya Mufindi
na kujikuta tunasonga mbele kwa upendo zaidi hivyo sisi kwa ajili
ya kumuenzi tutaanzisha mradi wa wanawake ambao utapewa jina la
Tasili Mgoda kama sehemu ya kumuenzi zaidi”
Mkini
ambae ni mjumbe wa NEC Taifa alisema kuwa kutokana kifo chake kuwa
ni histori kubwa ndani ya Taifa kwa mhasisi huyo wa TANU ambaye
alifanya kazi na baba wa Taifa kifo chake kutokea siku ambayo
ilikuwa ni kumbukumbu ya kifo cha mwalimu ni vema wana CCM kuendelea
kuenzi uzalendo na kuwakumbuka waasisi hao kwa kuepuka chuki ndani
ya chama na badala yake kudumisha umoja zaidi.
Alisema
pamoja na kuondoka kwa baba wa Taifa hivi sasa watanzania
wamepata tumaini jipya la uongozi unaofafana na ule wa mwalimu
Nyerere kwa kuwa na Rais Dkt John Magufuli ambae misingi yake ni sawa
kabisa na ya waasisi hao wa TANU hivyo ni vema kuzidi kumwombea na
kuendelea kuwaenzi waasisi waliotangulia kwa kufanya kazi zaidi.
Hivyo
alisema kutokana na Rais wa awamu ya tano Dkt Magufuli kuahidi
kutoa kiasi cha Tsh milioni 50 kwa kila kijiji ana amini wao kama UWT
wilaya ya Mufindi watakuwa ni mwanga wa kuhamasisha uanzishwaji wa
vikundi vya kiuchumi ambavyo vitanufaika na fedha hizo ili
kuwakumbuka waasisi hao na kutekeleza kauli mbiu ya hapa kazi Tu
kwa kufanya kazi bila kuchoka.
Kwa
upande wao wabunge walioshiriki katika mazishi hayo Mahamudu
Mgimwa wa Mufindi Kaskazini , Cosato Chumi wa Mafinga , Deo Sanga
kutoka mkoa wa Njombe Kaskazini
na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto walisema kuwa kuendelea kumuenzi
Mdoga ni kufanya kazi kwa umoja na kuepuka kutengana kwa misingi ya
kisiasa ama dini.
Huku
waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wilima Lukuvi ambae ni
mbunge wa jimbo la Ismani akisema kuwa misingi ya uongozi wake
marehemu Mgoda ndio ambao leo wananchi wa mikoa ya kusini
wanafurahia matunda yake ikiwemo lami ya Iringa – Dodoma na mengine
mengi ambayo ameyafanya kazi nafasi yake kama mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Iringa .
Viongozi wengine walijumuika katika mazishi hayo ni pamoja na naibu katibu mkuu wa CCM Bara Luhwavi , mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu na wengine pia Aliyekuwa mwenyeviti wa wenyeviti wa CCM, Pancras Ndejembi.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa alisema kuwa wazee wetu hao ambao wametangulia
mbele za haki uongozi wao hauonyeshi kama walikuwa wakifuata mikate
katika serikali ya Tanzania wala ndani ya CCM hivyo kuwataka wana
CCM kupunguza njaa katika kutumikia nafasi hizo na badala yake
kuungana kuijenga nchi na Chama bila kutanguliza njaa mbele.
Akisoma
wasifu wa marehemu Tasili Mgoda , Msambatavangu alisema kuwa Mgoda
alizaliwa July 6 1931 katika kijiji cha Mdandu wilaya ya Njombe
ambapo kwa sasa wilaya ya wanging’ombe kwa wakati huo kijiji cha
Mdandu ndicho kilikuwa makao makuu ya serikali ya Kikoloni wilaya ya
Njombe .
Elimu
Alipata
elimu ya Msingi shule ya msingi Kidugala kwa muda wa miaka miwili
kati ya mwaka 1942- 1943 baada ya hapo aliendelea na elimu ya msingi
Ilembula ambapo alisoma hadi darasa la sita mwaka 1947 alipohamia
sekondari ya Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi mwaka 1952
alihitimu kidato cha nne pamoja na masomo ya ufundi .
Mwaka
1973 Mgoda alikwenda nchini Marekani kupata mafunzo ya kilimo na
ufugaji ,aliwahi kupata mafunzo ya siasa na uongozi chuo cha
Kivukoni Dar es Salaam kwa sasa kinajulikana kama chuo cha kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere
Utumishi
Mwaka
1953 alianza kazi kama msimamizi wa kampuni ya Carpentry Furniture
iliyokuwa jijini Dar es salaam na mwaka 1956 aliamua kuachana na kazi
hiyo kwa kuwa alikuwa amejiunga na siasa akiwa ni mmoja wa vijana
wachache wa TANU waliokuwa na jukumu la kuhamasisha wananchi kukiunga
mkono chama cha TANu katika kutafuta UHuru wa Taifa letu ,mwaka
1957-1958 Mgoda alikuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya mkoa na wilaya
lakini pia akiwa ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya na mkoa.
Katika
uhai wake amepata kushika nafasi mbali mbali zikiwemo za ukuu wa
wilaya katika wilaya mbali mbali nchini katibu wa chama ,Mwenyekiti
wa chama mkoa wa Iringa na udiwani pia uenyekiti wa Halmashauri ya
Mufindi nafasi ambayo alidumu nayo hadi alipostaafu siasa.
No comments:
Post a Comment