Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya (kushoto)
aliyemtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Balozi wa Sudan nchini Mahgoub A. Sharfi (kushoto)
alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amesema serikali itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa
kihistoria kati ya Tanzania na India ambayo yamedumu kwa muda mrefu
hasa katika sekta mbalimbali ikiwemo za elimu,afya na biashara.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo 25-Okt-2016 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Sandeep Arya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais amesema mahusiano kati ya Tanzania na India yamesaidia kunufaisha wananchi wa
nchini mbili hasa katika masuala ya kibiashara,miradi ya maendeleo na
hivyo mahusiano hayo ni muhimu yakaendelezwa na kudumishwa.
Makamu wa
Rais katika mazungumzo na balozi huyo wa India hapa nchini Sandeep Arya
pia ameiomba serikali kuisaidia Tanzania katika mpango utakaosaidia
wakulima kupata taarifa mbalimbali zinazohusu kilimo na masoko ya bidhaa
zao kupitia simu za mkononi ili kuondoa usumbufu mkubwa wanaopata
wakulima kwa sasa hasa kuhusu masoko.
Kwa
upande wake, Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya amemhakikishia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
serikali yake itakuwa bega kwa bega na Tanzania katika kuhakikisha
wananchi wa pande Mbili wananufaika na mahusiano yaliyopo.
Balozi
Sandeep Arya amesisitiza kuwa serikali ya India itaendelea kuisaidia
Tanzania katika uimarishaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano
pamoja na miradi ya maendeleo na uimarishaji wa shughuli za kiuchumi.
No comments:
Post a Comment