Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli alipoingia madarakani mwezi Novemba 2015 aliendeleza
jitihada za kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kuweka mkazo na kutoa maagizo kwenye
maeneo kadhaa yakiwemo; kuongeza nguvu kwenye ukusanyaji wa kodi, kupiga vita rushwa,
kuweka msisitizo mkubwa wa nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, kupunguza matumizi
yasiyo ya lazima na kuelekeza matumizi katika sekta za vipaumbele vya maendeleo.
Aidha, kuzitaka Wizara, Wakala na Taasisi za Umma kuweka fedha zao Benki Kuu na
kuhimiza kila mtu afanye kazi na kula kwa jasho lake ili kutekeleza falsafa ya
‘Hapa kazi tu’.
Maagizo haya yamekuwa kichocheo cha ukuaji mzuri wa uchumi.
Kupitia maagizo haya Benki Kuu tunaweza kuelezea mafanikio kadhaa
yaliyopatikana katika kipindi hiki kama ifuatavyo;
1. Kuimarisha
ukusanyaji wa mapato, kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kuelekeza matumizi katika
sekta za vipaumbele vya maendeleo
·
Tangu Serikali
ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani mnamo Novemba mwaka 2015, makusanyo ya
mapato yameendelea kuongezeka. Kwa mfano, kati ya Januari hadi Septemba 2016,
makusanyo ya mapato ya ndani yalikuwa shilingi bilioni 11,174 ikiwa ni wastani
wa shilingi bilioni 1,241.55 kwa mwezi, ikilinganishwa na wastani wa shilingi
bilioni 950.22 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2015. Makusanyo ya mapato ya
ndani katika 2016 yalitosheleza matumizi yote ya kawaida (recurrent) na
kubakiza ziada kwa ajili ya ulipaji wa madeni ya nje (amortization) na sehemu
kubwa ya matumizi kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Ukuaji wa Pato la Taifa (Real GDP)
·
Uchumi umeendelea kukua kwa kiwango kikubwa kutokana na sera nzuri za
uchumi mpana (macroeconomic policies). Kasi ya ukuaji wa pato la
Taifa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, yaani Januari-Juni 2016, imeongezeka
na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya
mwaka 2015.
Ukuaji huu umechangiwa na kukamilika kwa bomba la gesi kutoka Mtwara
hadi Dar
es Salaam na kuanza kutumia gesi katika kuzalisha
umeme, usafirishaji, ukiwemo usafiri wa abiria kutumia reli na mabasi ya
mwendo kasi (UDART);
kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi, uzalishaji wa gesi, vyuma na
bidhaa
zisizo za vyuma pamoja na kuimarika na kupanuka kwa huduma za kifedha.
Sekta za uchumi zilizoongoza katika kasi ya ukuaji ni usafirishaji
(asilimia 17.4), madini (mining and quarrying) (13.7), fedha na bima
(asilimia
8.7), uzalishaji viwandani (manufacturing) (asilimia 8.3) na elimu
(asilimia
8.0) kutokana na sera ya utoaji wa elimu ya msingi bila malipo iliyoanza
Januari 2016.
Mfumuko wa bei
Mfumuko wa bei ulibakia katika kiwango cha tarakimu moja (single digit)
kutokana na sera nzuri ya fedha na ile ya bajeti pamoja na kupungua kwa bei za
bidhaa duniani kote. Katika mwaka ulioishia Septemba 2016, mfumuko wa bei
ulikua kwa asilimia 4.5 ikilinganishwa na asilimia 6.1 kaitka kipindi kama
hicho mwaka 2015 na lengo la muda wa kati la asilimia 5.0. Kutokana na sera za
uchumi mpana, pamoja na kuimarika kwa shilingi dhidi ya dola ya Marekani na bei
ndogo za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei unatarajiwa kubakia karibu
na lengo la kiwango cha muda wa kati cha asilimia 5.0.
Shughuli za Serikali
·
Serikali ya
awamu ya tano ilianza katika kipindi ambacho upatikanaji wa misaada ya kibajeti
(GBS) ulikuwa siyo mzuri kutokana na kubadilika kwa sera za maendeleo za
kimataifa (foreign development policies) katIka nchi wahisani ambapo mwelekeo
ulikuwa ni kupeleka fedha za miradi moja kwa moja. Pamoja na nchi nyingi
wahisani kujitoa katika kusaidia katika bajeti (GBS), Serikali ya awamu ya tano
imeweza kushirikiana na wadau wa maendeleo (DPs) katika kutafuta njia mbadala
za kuziba pengo hilo.
2. Uimarishaji
Wa Ukusanyaji Wa Mapato Uliendana Na Uimarishaji Wa Mazingira Mazuri ya Kibiashara
·
Sera nzuri za uchumi
(macroeconomic policies) za awamu ya tano zimeendelea kukwamua na kuimarisha
mazingira ya biashara. Hii imejidhihirisha
katika kuimarika kwa nakisi katika urari wa biashara (current account deficit)
katika miezi tisa ya mwazo ya 2016. Nakisi ya urari wa biashara imepungua sana,
kufikia dola za Marekani millioni 1,621.8 katika mwezi tisa ya 2016 kutoka nakisi
ya dola milioni 3,715.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Hii ni kutokana
na kuongezeka kwa mauzo ya nje ya bidhaa na huduma (utalii, dhahabu, bidhaa za
viwandani), pamoja na kupungua kwa kiwango kikuwa kwa uagizaji wa bidhaa na
huduma (mitaji, mafuta, chakula na bidhaa za chakula).
Thamani ya
Shilingi
·
Kutokana na sera
nzuri za Serikali ya Awamu ya Tano, thamani ya shilingi imebaki kuwa imara (wastani
wa shilingi 2,178.6 kwa dola ya Marekani) ikilinganishwa na dola ya Kimarekani
na sarafu zingine za nchi jirani na nchi washirika wa kibiashara. Kutokuyumba
kwa shilingi kumechangiwa na kuimarika kwa uchumi; kuhamishwa kwa fedha za
mashirika ya umma kutoka mabenki ya biashara kwenda Benki Kuu; kupunguzwa kwa
matumizi yasiyo ya lazima ya Serikali na kutoterereka kwa Akiba ya Fedha za Kigeni.
Akiba ya Fedha za Kigeni
·
Akiba ya fedha
za kigeni imebaki kuwa imara, ikiwa ni dola za Marekani milioni 4,096.0 kufikia
mwisho wa mwezi Septemba 2016, ambao ni uwezo wa kutosheleza uagizaji nje wa
bidhaa na hudumu kwa kipindi cha miezi 4. Kuongezeka (kutotetereka) kwa Akiba
ya Fedha za Kigeni kunatokana na manunuzi yanayofanywa na Benki Kuu kutoka
kwenye soko la ndani la fedha za kigeni na mashirika ya umma.
3. Kuhamisha
Fedha za Mashirika ya Umma kutoka katika Mabenki Binafsi kwenda Benki Kuu ya Tanzania
Serikali ya Awamu
ya Tano iliagiza utekelezaji wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, hasa Sura ya
32 inayohusu utunzaji wa amana za mashirika ya umma na taasisi za serikali.
Imechukua miaka tisa kuanza kutekeleza masharti ya hiyo kuhusu akaunti za Mashirika
ya Umma, Idara za Serikali na Serikali za Mitaa. Kuchelewa huku, kulizifanya
benki nyingi za biashara zitumie fedha hizo za umma kununua Dhamana za Serikali
na Hati Fungani na hivyo kuifanya Serikali kuuziwa fedha zake yenyewe. Biashara
hiyo sasa imekoma kutokana na hatua madhubuti za kuitekeleza sheria hiyo.
Hatua hizo
zimewezesha kupatikana na kwa mafanikio yafuatayo:
(a) Kufungua
akaunti za amana za Mashirika ya Umma na Idara za Serikali: Kati ya Novemba
2015 hadi Oktoba 26, 2016, jumla ya akaunti 267 zenye jumla ya amana za
Shilingi 206,913,915,522.06 zimefunguliwa.
Aidha, baadhi ya taasisi hizo zimefungua akaunti za fedha za kigeni 131 zenye
Dola 163,480,125.75, sawa na
shilingi 357,694,000,000.00. Hivyo
jumla ya amana zote za shilingi na fedha za kigeni za mashirika na taasisi za
umma zinazotunzwa Benki Kuu ni shilingi 564,608,460,663.00
(b) Amana za akaunti za Serikali za
Mitaa: Serikali imeamua kufungua akaunti maalum kwa ajili
ya kutunza amana za Serikali za Mitaa. Mradi huu umeanza kutekelezwa kuanzia
mwezi Aprili 2016 na mpaka sasa jumla ya mikoa mitano imeunganishwa. Mikoa hiyo
ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Mpaka tarehe 26 Oktoba 2016,
amana za halmashauri za mikoa hiyo mitano ambazo zipo Benki Kuu ya Tanzania zinafikia
kiasi cha shilingi 108,387,942,351.15. Bila
kukamilisha sehemu ya mradi huu, fedha hizi zingekuwa kwenye benki za biashara.
Matokeo:
·
Kwa upande Serikali;
·Kumeleta uwazi
kuhusu mapato na matumizi ya mashirika hayo
·Kupungua kwa
gharama za usimamizi wa ujazi wa fedha (liquidity management) kwenye mzunguko.
·
Kwa mabenki;
·kumeleta usawa
katika ushindani kati ya mabenki badala ya wachache kunufaika kwa kupata amana
za mashirika ya umma.
·kumeleta ubunifu
kwa mabenki katika kubuni bidhaa (bank products) mbali mbali mpya ili
kujiongezea amana.
·Kutokana na Sera
ya Fedha ambayo ni rafiki, malengo mapana ya Serikali, ukuaji wa uchumi na
ukuaji wa fedha ukuwa ndani ya malengo.
·Katika kipindi
cha miezi tisa ya 2016, amana katika mabenki ya biashara zimeongeza kutoka
asilimi 9.84 katika miezi tisa ya mwanzo wa mwaka 2015 na kufikia asilimia
11.59 kaitka miezi tisa yam waka 2016. Vile vile, riba za mikopo kwa mwaka
mmoja zilipungua kutoka wastani wa asilimia 15.49 na kufikia asilimia 13.87
·Mwenendo huu wa
riba ulipelekea kupungua kwa tofauti kati ya riba za mkopo na zile za amana
kutoka wastani wa asilimia 5.92 ilivyokuwa katika miezi tisa ya mwanzo ya 2015
na kufikia wastani wa asilimia 2.28 katika miezi tisa ya 2016, ikimaanisha
kupugua kwa gharama za mikopo.
Mafanikio mengine
4. Mwenendo wa Sekta ya Kibenki
Katika kipindi cha kuanzia Septemba 2015 hadi September 2016,
sekta ya kibenki imeendelea kukua ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa taasisi
mpya za kifedha ikiwemo Benki ya Waalimu Tanzania (Mwalimu Commercial Bank Plc)
na Canara Bank (Tanzania) Limited. Takwimu zinaonesha kuwa mabenki yetu ni
imara na salama, yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha. Kufikia mwezi Septemba
2016, kulikuwa na jumla ya benki na taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki
Kuu zipatazo 66 zenye matawi 750 nchini kote, ikilinganishwa na taasisi 62
zilizokuwa na matawi 715 mwezi Septemba 2015.
Katika kipindi hicho, benki mbili - Guaranty Trust Bank Tanzania Ltd na Yetu Microfinance Bank Plc na taasisi ya fedha moja ya M Mortgages Tanzania Ltd zilipata leseni za muda.
Katika kipindi hicho, benki mbili - Guaranty Trust Bank Tanzania Ltd na Yetu Microfinance Bank Plc na taasisi ya fedha moja ya M Mortgages Tanzania Ltd zilipata leseni za muda.
Kiwango cha mitaji kikilinganishwa na mali iliyowekezwa (total
capital to total risk weighted assets and off-balance sheet exposures)
kilikuwa asilimia 19.24 kikilinganishwa na kiwango cha chini kinachotakiwa
kisheria cha asilimia 12. Hali ya ukwasi, ambayo hupimwa kwa kuangalia uwiano
kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza
kuhitajika katika muda mfupi (liquid assets to demand liabilities),
ulikuwa asilimia 34.18 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria
wa asilimia 20.
Mpaka kufikia Septemba 2016, mikopo chechefu ilikuwa wastani wa asilimia
9.06 ikilinganisha na wastani wa asilimia 6.61 ya Septemba 2015. Mikopo
chechefu imeendelea kuwa ni changamoto katika sekta ya kibenki kutokana na
ufanisi mdogo wa urejeshaji mikopo katika sekta ya kilimo na biashara.
Amana za wateja katika mabenki zilipungua kutoka shilingi trilioni
20.19 mwezi Oktoba 2015 hadi kufikia shilingi trilioni 20.01 mwezi Septemba
2016. Miongoni mwa sababu zilizochangia kupungua kwa amana kwenye mabenki ni
pamoja na uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika
ya umma kutoka mabenki ya biashara kwenda Benki Kuu ya Tanzania. Aidha, mikopo
(loans and overdafts) iliongezeka
kutoka shilingi za Kitanzania trilioni 14.48 mwezi Oktoba 2015 hadi kufikia
shilingi trilioni 15.74 mwezi Septemba 2016.
Jumla ya rasilimali (Total assets) za mabenki na taasisi za fedha ziliongezeka
kwa asilimia 4.71 kutoka shilingi trilioni 26.57 mnamo Septemba 2015 mpaka shilingi
trilioni 27.82 mwisho wa Septemba 2016. Kwa kipindi cha miezi tisa kufikia
Septemba 2016, jumla ya faida baada ya kodi katika sekta ya kibenki iliongezeka
kufikia shilingi trilioni 352.37 ikilinganishwa na shilingi trilioni 344.87 katika
kipindi kilichoishia Septemba 2015.
Upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi umeendelea
kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia katika utoaji wa
huduma za malipo ya rejareja kupitia simu za mkononi, pamoja na huduma za
kibenki kupitia mawakala (agent banking services).
Mabenki
yameendelea kutumika katika kutunza fedha na mitaji ya wateja na kurahisisha
miamala au malipo kwa wateja wake. Ili kulinda maslahi ya wateja na amana zao,
Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutunga sheria, kanuni na miongozo inayotumiwa
na mabenki na kusimamia utekelezaji wake.
Katika kipindi husika, Benki Kuu ya Tanzania imeendelea
na jukumu lake la kusimamia
na kudhibiti mabenki na taasisi za fedha kwa niaba ya Serikali ya
Tanzania. Benki Kuu, imeendelea kuhakikisha kuwa mabenki na taasisi za fedha zina
mikakati inayokidhi vigezo muhimu (minimum standards) kwa kupitia ukaguzi wa
mabenki unaofanyika mara kwa mara.
Maduka ya Kuuza Fedha
za Kigeni
Idadi
ya Maduka ya Kuuza Fedha za Kigeni (bureaux de change) imefikia 290
ikilinganishwa na maduka 266 yaliyokuwepo Septemba 2015. Mpaka kufikia Septemba
2016, maduka yapatayo 260 yalikuwa yanafanya biashara Tanzania Bara na 30
Tanzania Visiwani, ikilinganishwa na maduka 239 Tanzania Bara na 27 Tanzania
Visiwani yaliyokuwa yanafanya biashara kufikia Septemba 2015.
Benki Kuu inasimamia
usalama, utulivu na uthabiti wa sekta ya benki Tanzania. Inalinda wateja
wanaoweka amana zao kwenye mabenki na taasisi za fedha. Mabenki yanaendelea kutoa mchango mkubwa
kwenye kukuza uchumi wa nchi; kuongeza ushindani kwenye sekta ya kibenki na kuzuia
matumizi mabaya ya sekta ya kifedha. Benki Kuu imeendelea kupima ustahimilivu
wa mabenki wakati inapojitokeza hali ambayo inaweza kuathiri mapato na mitaji
ya mabenki hayo (Stess testing). Pia, husaidia katika kutoa mwelekeo wa Sera ya
kifedha nchini.
Sekta ya kibenki imeendelea kushuhudia mabadiliko makubwa
katika aina za huduma zitolewazo na katika njia zinazotumika kutoa huduma hizo.
Mabadiliko hayo ni pamoja na; Huduma za kibenki kwa kufuata misingi ya Shariah;
Huduma za kibenki kupitia wakala; Huduma za kifedha kupitia simu za mikononi na
Benki Kuu imeendelea kusimamia benki mbili za maendeleo
(TIB na TADB) ili ziweze kutoa mikopo katika sekta mbalimbali na kuweza
kuharakisha maendeleo hapa Tanzania.
Mfumo wa Upashanaji wa Taarifa za Wakopaji
Mfumo wa upashanaji taarifa za wakopaji umeendelea kuleta
mafanikio makubwa katika kuboresha upatikanaji wa mikopo kutoka kwenye mabenki
na taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu, pamoja na taasisi nyingine
zinazotoa mikopo(SACCOS, MFIs, Utility Companies, Car Dealers na HESLB).
Mfumo huo unajumuisha utaratibu wa kuweka taarifa za wakopaji kupitia Benki Kuu (Credit reference databank), na makampuni binafsi yaliyoruhusiwa kubadilishana taarifa za wakopaji na mabenki na taasisi nyingine zinazotoa mikopo. Kufikia Septemba 2016 jumla ya wakopaji waliokuwa katika mfumo huo walikuwa zaidi ya 1,600,000 ikilinganishwa na zaidi ya 900,000 ya Septemba 2015.
Jumla ya mikopo mpaka kufikia Septemba 2016 ilikuwa ni zaidi ya 3,000,000 ukilinganisha na zaidi ya 1,690,000 ya Septemba 2015. Katika taarifa ya mazingira ya biashara (World Bank Doing Business Report, 2017), Tanzania imefanya vizuri kutoka nafasi ya 152 hadi 44 kati ya nchi 190 zilizofanyiwa utafiti huo.
Mfumo huo unajumuisha utaratibu wa kuweka taarifa za wakopaji kupitia Benki Kuu (Credit reference databank), na makampuni binafsi yaliyoruhusiwa kubadilishana taarifa za wakopaji na mabenki na taasisi nyingine zinazotoa mikopo. Kufikia Septemba 2016 jumla ya wakopaji waliokuwa katika mfumo huo walikuwa zaidi ya 1,600,000 ikilinganishwa na zaidi ya 900,000 ya Septemba 2015.
Jumla ya mikopo mpaka kufikia Septemba 2016 ilikuwa ni zaidi ya 3,000,000 ukilinganisha na zaidi ya 1,690,000 ya Septemba 2015. Katika taarifa ya mazingira ya biashara (World Bank Doing Business Report, 2017), Tanzania imefanya vizuri kutoka nafasi ya 152 hadi 44 kati ya nchi 190 zilizofanyiwa utafiti huo.
Mifumo ya Malipo Nchini
Benki Kuu imeendelea na kazi yake ya kisheria ya
kusimamia mifumo ya malipo nchini ambapo Sheria ya Mifumo ya Malipo Nchini 2015
imeanza kufanya kazi. Chini ya sheria hii zimeanzishwa kanuni mbili za
uendeshaji wa mifumo. Kanuni hizo ni pamoja na Kanuni ya Leseni na Vibali kwa
Watoa Huduma za Mifumo ya Malipo 2015 pamoja na Kanuni za Kutoa Fedha za
Kielektroniki 2015. Uwepo wa Sheria
umeimarisha usalama katika mifumo ya malipo nchini na kuongeza ufanisi katika
usimamizi wa mifumo ya malipo ya taifa.
Kwa kipindi hiki, huduma za fedha jumuishi
(financial inclusion) imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikichangiwa na usalama
uliopo kwenye mifumo ya malipo. Aidha, idadi ya watumiaji wa huduma za fedha
kwa njia ya mtandao imeendelea kuongezeka kwa kasi kubwa.
Kutokana na maendeleo haya, wananchi wamefaidika kwa kupata huduma mbali mbali za kifedha kama vile, kutuma na kupokea, kutunza fedha, huduma za bima, huduma za mikopo midogo midogo. Kadhalika, huduma za malipo ya ada mbali mbali kama vile ada za shule, kodi ndogo ndogo, faini ya makosa ya barabarani na malipo ya huduma kama za maji, umeme na televisheni. Benki kuu inaendelea kushirikiana na wadau wengine wa serikali ili kuahakikisha kuwa mifumo hii ya malipo pia inatumiwa katika kukusanya mapato ya serikali.
Kutokana na maendeleo haya, wananchi wamefaidika kwa kupata huduma mbali mbali za kifedha kama vile, kutuma na kupokea, kutunza fedha, huduma za bima, huduma za mikopo midogo midogo. Kadhalika, huduma za malipo ya ada mbali mbali kama vile ada za shule, kodi ndogo ndogo, faini ya makosa ya barabarani na malipo ya huduma kama za maji, umeme na televisheni. Benki kuu inaendelea kushirikiana na wadau wengine wa serikali ili kuahakikisha kuwa mifumo hii ya malipo pia inatumiwa katika kukusanya mapato ya serikali.
Aidha, kuanzia Februari 2016, Tanzania imekuwa nchi
ya kwanza duniani kuweza kufanikisha malipo ya moja kwa moja kutoka mtandao
mmoja kwenda mwingine (wallet to wallet interoperability). Mafanikio haya
yatawezesha wananchi kupata huduma za kifedha kwa mtandao kwa urahisi na unafuu
zaidi.
Uboreshwaji wa huduma za malipo ya serikali kwa
njia ya kieletroniki kama mbadala wa malipo kwa njia ya cheki za serikali,
baada ya kuanzisha mfumo maalumu wa malipo ya serikali ambayo unasaidia sasa
serikali kulipa mishahara, pensheni pamoja na mirathi bila kutumia cheki. Mfumo
huu umesaidia kuleta uharaka na usalama katika malipo ya serikali na kupunguza
mianya ya wizi uliokuwa unafanywa na wahalifu kutokana na mapungufu ya mfumo wa
utoaji wa cheki za serikali. Aidha ili kusaidia malipo ya mishahara, Benki kuu
pia iliongeza kiwango cha ukomo wa malipo kwa njia ya kutumiana kwenye akaunti
za kibenki (Electronic Fund Transfer (EFT)) kutoka Milioni Kumi (10,000,000) ya
awali hadi Milioni Ishirini (20,000,000/=) ili kuiwezesha serikali kulipa
malipo mengi zaidi kwa njia hii.
Ili kuongeza matumizi ya malipo kwa njia ya
kieletroniki katika halimashauri, Benki kuu iliamua kuunganisha halmashauri
kwenye mfumo wa Malipo wa TISS (Tanzania Interbank Settlement System (TISS).
Hadi sasa halmashauri zote katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza (isipokuwa
Ilemela and Buchosa), Arusha, Mbeya (isipokuwa Busekelo), Dodoma (isipokuwa
Kondoa and Chemba) na Songwe (isipokuwa Songwe and Tunduma)
zimekwishaunganishwa, pamoja na hazina ndogo zote 24. Hali hii imesaidia
kuongeza udhibiti wa malipo ya serikali pamoja na ufanisi katika ulipaji, hali
ambayo imesaidia serikili kwa kiwango kikubwa kutekeleza malengo yake.
Katika juhudi za serikali kurahisisha na kuleta
ufanisi katika ukusanyaji wa kodi na maduhuli mbali mbali, Benki Kuu imeendelea
kufanikisha unganishwaji wa watoa huduma mbali mbali katika mifumo yake ya
malipo. Kwenye mfumo wa TACH, Benki kuu imefanikiwa kuongeza Benki nne (4)
tangu katika kipindi kifupi ambazo ni TIB Corporate Bank (December 2015),
Tanzania Postal Bank (April 2016), Canara Bank Tanzania Ltd (September 2016) na
Mwalimu Commercial Bank Plc (October 2016). Aidha, kwenye mfumo wa TISS, Benki
Tatu (3) zaidi zimejiunga ambazo ni Canara Bank Tanzania Ltd , Meru Community
Bank na Mwalimu Commercial Bank Plc.
Kujiunga kwa Benki hizi kwenye mifumo ya malipo ya Benki kuu, imeongeza wigo wa
watoa huduma walio tayari kukusanya mapato ya serikali sehemu mbali mbali.
Ili kuunga mkono juhudi za serikali za kukusanya
kodi na mapato mengine, Benki kuu imeongeza muda wa kuendesha mifumo yake ili
kuwangezea walipaji muda zaidi wa kufanya malipo kupitia mifumo hii. Muda wa
mfumo wa TISS kufanya kazi umeongezwa
kutoka saa 10 jioni hadi saa 2 za usiku. Aidha sasa hivi mfumo huu unafunguliwa
pia siku za jumamosi na jumapili kinyume na hapo awali.
Benki kuu imeendelea kushirikiana na nchi nyingine
za jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla ili kutengeneza na
kuendeleza mifumo ya malipo inayovuka mipaka. Mfumo wa malipo wa Afrika
Mashariki (East African Cross Border Payment System) umeendelea kuboreshwa ili
uweze kutumiwa zaidi na wananchi wanaofanya malipo ndani ya nchi za jumuiya ya
Afrika Mashariki. Katika kipindi hiki, malipo yanayopita kwenye mfumo huu
yamezidi kuongezeka, hususa ni yale yanayofanywa kati ya Tanzania na Kenya.
Mifuko ya Udhamini wa Mikopo
Benki Kuu,
ambayo ni wakala wa Serikali kupitia Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, husimamia
Mifuko ya Udhamini wa Mikopo itolewayo na mabenki kwa sekta binafsi pamoja na
sekta zinazojihusisha na uzalishaji na uuzaji wa mazao nje ya nchi. Kwa sasa
Benki Kuu inasimamia mifuko miwili ambayo ni Mfuko wa Udhamini wa Mauzo Nje ya
Nchi (ECGS) na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa kati
(SME-CGS).
Katika kipindi
cha Novemba 2015 mpaka Oktoba 2016 dhamana zenye thamani ya:
-
Shilingi 130,867,038,874.85 zilitolewa
chini ya Mfuko wa Udhamini wa Mauzo Nje ya Nchi (ECGS). Kupitia mfuko huu,
mabenki yameweza kukopesha vyama vikuu vya Ushirika na vya Msingi
vinavyojishughulisha na ununuzi wa mazao na pembejeo za kilimo. Hali kadhalika;
na
-
Shilingi 918,318,215 zilitolewa chini ya
Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa kati (SME-CGS).
Mikopo hiyo ilitolewa kwenye sekta za kilimo na ujenzi.
Huduma za Kibenki
Uharaka
wa malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali:
Kwa karibu kipindi cha miezi 11 sasa tangu Novemba 2015, mishahara imekuwa
ikilipwa kwa wakati na mara nyingi imekuwa ikilipwa kabla ya tarehe 25 ya mwezi
husika ikilinganishwa na siku za nyuma.
Kuchelewa kulipa
mishahara kumekuwa kukitokana na uhaba wa fedha hasa baada ya ukomo wa kukopa
kufikia mwisho. Hii haikuwa mwenendo mzuri kwani wafanyakazi hawakuwa na
uhakika wa siku ya kulipwa mshahara.
Kuongezeka
kwa matawi ya Benki Kuu: Moja ya majukumu ya Benki Kuu ya
Tanzania ni kusambaza fedha katika matawi yake. Hadi June 2016, Benki Kuu
ilikuwa na matawi matano, nayo ni; Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar na Dodoma.
Kwa vile
Tanzania ina eneo kubwa; shughuli hii imekuwa na changamoto za usambazaji wa
noti na sarafu katika maeneo ambayo Benki Kuu haina matawi yake. Ili
kukabiliana na changamoto hii Benki Kuu imesaini mikataba na mabenki ya
biashara ya usambazaji wa noti na sarafu kama ifuatavyo: -
(i) Benki ya CRDB katika mikoa ya Mtwara,
Kigoma, Sumbawanga, Songea na Tanga
(ii) NMB katika mkoa wa Tabora
(iii) NBC katika mikoa ya Shinyanga na Bukoba
(iv)
PBZ katika kisiwa cha Pemba
Vituo hivi vyote
vimekuwa vikifanya kazi kwa ufanisi; lakini kumekuwa na changamoto mbalimbali;
kubwa ikiwa ni udogo wa maghala yake kuhifadhi mahitaji halisi ya noti na
sarafu kwa muda muafaka. Hali hii huilazimisha Benki Kuu kupeleka pesa mara kwa
mara na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji.
Kutokana na
changamoto hizi, Benki Kuu imejenga tawi jipya katika mkoa wa Mtwara ambalo
limeanza kazi rasmi mefunguliwa tarehe 3 Octoba 2016. Benki Kuu inaamini kuwa
tawi hili jipya litakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwenye eneo la kusini
mwa Tanzania.
Miradi
mikubwa ya viwanda na miundombinu inayoendelea na inayotarijiwa kuanza kazi
siku za usoni itachangia katika kuimarisha uchumi.
- Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge)
- Ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda ambalo litahusu vile vile upanuzi wa bandari ya Tanga
- Ujenzi wa Export Processing Zone ya Kurasini – itakayokuwa mhimili wa biashara kati ya China na Ukanda huu wa Afrika
- Mradi wa kuzalisha megawati 240 za umeme wa Kinyerezi II unaoendelea kujengwa.
- Miradi ya kupanua viwanja vya ndege nchini kwa mfano- Dodoma, na mingine inayoendelea -katika viwanja vya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya n.k.
- Ujenzi wa maghala ya taifa ya kuhifadhi chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 350 yatakayojengwa kwa msaada wa Serikali ya Hungary katika sehemu mbalimbali nchini hususan katika mikoa inayozalisha mazao ya nafaka kwa wingi.
- Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara ambacho kipo mbioni kuzalisha kulingana na uwezo wake (full capacity);
- Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Mkuranga, Pwani ambacho ujenzi wake unaendelea
- Kiwanda cha kuzalisha mbolea mkoani Lindi - kinajengwa
- Kiwanda cha bidhaa za chuma – mkoani Pwani ambacho kiko mbioni kukamilika.
Hitimisho
Maagizo mbali
mbali yaliyotolewa na Serikali
ya Awamu ya Tano yamechochea ukuaji wa
uchumi katika kipindi cha mwaka
mmoja uliopita. Mwenendo wa viashiria
mbalimbali vya shughuli za uchumi unadhihirisha kwamba hali ya uchumi wa
Tanzania ni nzuri na inatoa matumaini makubwa. Matarajio ni kwamba endapo shughuli
halali za kiuchumi zitaendelea kutekelezwa, lengo la ukuaji wa pato la Taifa la
asilimia 7.2 kwa mwaka 2016 litafanikiwa. Hii inachangiwa pia na ukweli kwamba
serikali ya awamu ya tano imejipanga katika kuimarisha uchumi endelevu usiokuwa
na mianya ya rushwa; usimamizi thabiti wa rasilimali za umma; na ujenzi wa
miundombinu bora kwa lengo la kujenga uchumi wa viwanda chini ya Mpango wa
Maendeleo wa Miaka Mitano.
No comments:
Post a Comment