MKUU wa
wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama akizungumza na madiwani na watendaji
wa halmashauri ya Mji wa Kibaha katika kikao cha baraza la madiwani
.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Diwani wa viti maalum Tuaje Ponza,akizungumza jambo katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Kibaha .
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MADIWANI
wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha ,wamesikitishwa na kushuka kwa makusanyo
ya mapato ya ndani yanayotokana na ushuru wa stendi ya mabasi
Mailimoja,Machinjio na Mchanga na wakihofia huenda kuna hujuma
inafanyika.
Mapema
mwezi agosti ,halmshauri hiyo ilidai inatarajia kuokoa kiasi cha
sh.mil.516.792 katika mwaka wa fedha 2016/2017,zilizokuwa zikipotea
katika makusanyo ya vyanzo hivyo kutokana na udanganyifu wa baadhi ya
mawakala.
Wakizungumza
katika kikao cha madiwani,baadhi ya madiwani hao,diwani wa kata ya
Tumbi, Hemed Chanyika ,diwani wa viti maalum Selina Wilson na Tuaje
Ponza walishangaa makusanyo hayo kushuka zaidi ukilinganisha na
ukusanyaji uliokuwa ukifanywa na mawakala wasio wa serikali.
Aidha
walisema madiwani waligundua kuna ubabaishaji kipindi cha nyuma ambapo
halmashauri ingeokoa mil.335.392 zilizokuwa zikipotea kwa mwaka kwenye
ushuru wa mchanga.
Walieleza
katika ushuru wa mchanga walikuwa wakipokea mil.264.608 kwa mwaka baada
ya kutuma madiwani waligundua watakuwa wakipata mil.600 kwa mwaka.
Chanyika
alifafanua, katika ushuru wa stendi ,halmashauri ilikuwa ikipokea
makusanyo ya Sh.mil.320 kwa mwaka baada ya uchunguzi wa madiwani
wakabaini kuwa wangepata mil.458 kwa kipindi hicho na kuokoa mil 138
zilizokuwa zikipotea.
Alisema
kuanzia hapo ndipo halmashauri ilianza kutumia vibarua watakaokuwa
wanakusanya ushuru wa vyanzo hivyo kwa usimamizi wa watendaji wa
halmashauri badala ya mawakala .
“Matokeo
yake mambo yanaenda ndivyo sivyo ,mapato yanayotokana na vyanzo vya
mapato vya stendi na mchanga sasa yanashuka siku hadi siku tofauti na
ilivyokuwa kipindi cha nyuma ”
“Stendi
ni ile ile mabasi ni yale yale lakini tangu tenda irudi serikalini
mapato ndio yanadidimia kila mwezi sasa hatujui kuna hujuma ili tenda
hii irudi kwa mawakala ama”alisisitiza Chanyika.
Tuaje
Ponza alisema wastani kwa mwaka waliojiwekea ni kukusanya mil 458 katika
ushuru wa stend ambapo kwa mwezi ni wastani wa mil.35-40 lakini
haifikii lengo kwani wanakusanya mil.27 hadi 30 .
Hata hivyo alieleza,ushuru wa mchanga makisio ilikuwa ni kukusanya sh.mil.
600 kwa mwaka na kwa mwezi ilitakiwa wakusanye mil.50 na badala yake
wanapata mil 21-31 sawa na asilimia 15 ambayo haifikii malengo ya
asilimia 80.
Selina Wilson alitaka kujua mpango utakaofanywa ili kukerekebisha hali hiyo hatimae kunusuru vyanzo hivyo.
Alisema chanzo cha stendi ya mabasi ni muhimu,kinastahili kupewa kipaombele hivyo utata uliopo ufuatiliwe bila mzaha.
Akizungumzia
chanzo cha machinjio ,Selina aliomba huduma ya maji ipelekwe na
isichukue muda ili machinjio hayo yaweze kujiendesha na halmashauri
ipate mapato yakutosha.
Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha,Amkawane Ngilangwa ,alikiri
ni kweli mapato yanaonekana kushuka hasa kutokana na mabasi mengine
kukwepa kuingia stendi.
Alisema
kwasasa wamejiwekea mkakati wa kufuatilia kwa mkuu wa kituo cha polisi
Kibaha(OCD) na askari wa usalama barabarani Mailmoja pamoja na kusimamia
na kuhakikisha mabasi yote yanaingia stend ili chanzo hicho kiendelee
kuongeza mapato.
Katika
hatua nyingine mweka hazina wa halmashauri ya Mji wa Kibaha,Suzana
Chaula, alisema ni kweli ushuru wa mchanga haupatikani kama inavyotakiwa
kutokana na mchanga unaotoka nje ya halmashauri hiyo huwa hautozwi
ushuru na baadhi ya machimbo yanafungwa .
Alisema
tayari menejimenti imefanyia kazi kwa kushirikiana na madiwani
,wenyekiti wa mitaa na watendaji wa kata,kupata takwimu halisi ya
machimbo ya mchanga mara kwa mara.
Suzana
alisema menejiment pia imeunda timu ya wataalamu wa kufuatilia kwa kina
suala la mchanga na kuteua msimamizi kwenye ushuru wa mchanga .
Mkuu wa
wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama alisema hawezi kuliachia suala hilo
atafuatilia kujua chanzo kinachosababisha kuzorota kwa mapato hayo .
Alisema
haiwezekani kuona serikali inakusanya mapato hafifu wakati mawakala
wasio wa serikali walikuwa wakikusanya mapato kwa kiwango
kinachoridhisha.
Assumpter
alisema inashangaza serikali haina meno na uwezo wa kukusanya kodi na
kushuka kuliko makampuni ,kwa hilo hawezi kulifumbia macho.
“Nina
wasiwasi kuna hujuma inafanyika ama kuna watu ambao wanaweka fedha
mifukoni,nataka kupewa jibu kwanini makusanyo yameshuka,na iwekwe
mkakati kuwa ni lazima mabasi yote yaingie stendi’alisema Assumpter.
Aliwataka
wasimamizi wawe macho ili fedha ikusanywe ipasavyo na kumtaka OCD
asimamie suala hilo na endapo ikigundulika kuna mabasi yanaendelea
kupita bila kulipia ushuru askari aliyekuwepo zamu aondoke.
No comments:
Post a Comment