Thursday, October 27, 2016

Maagizo 10 ya Makamba kwa uongozi wa mkoa wa Katavi baada ya kukamilisha ziara

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo aliangalia mradi Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda ambao kwasasa umesitisha kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha katika Mto Katuma.

Katika kikao cha Majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:

1. Ongezeko la watu na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira.

2. Kusitisha uchepushaji kwa Mto Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla yamabanio 40 ambayo yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.

3. Uchimbaji hatari wa Madini usiofuata taratibu

4. Kuhuisha sheria ndogo ndogo za mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa

5. Kuanisha maeneo maalumu ambayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingiranyeti ili kuyapa ulinzi zaidi

6. Kusimamia uondoshwaji wa wavamizi katika Vyanzo vya maji

7. Kufanyika kwa sensa ya mifugo ili kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna boraya kuhumudimia mifugo hiyo bila kuathiri mazingira

8. Ameahidi kuaanda andiko maalumu la Mradi wa Ziwa Katuma

9. Mmiliki wa Jema Sitalike Project kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini isitishwe,apigwe faini na kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa shughuli za uchenjuaji wadhahabu.

10. Waziri Makamba meagiza Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini bila kufuata utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha Waziri Makamba amewasili Katika Mkoa wa Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines nakuwapongeza kwa kuzalisha chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho kilifungiwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na uharibifu wa Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment