Rais
mstaafu kutoka kwenye awamu ya nne ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Jakaya Mrisho Kikwete ameamua kujibu kile kinachoendelea kwenye mitandao
ya kijamii katika siku za karibuni.
Usiku
wa kuamkia leo, kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Mstaafu wa
Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete aliandika masikitiko yake juu ya namna watu
wanavyotumia picha zake na kupotosha yale aliyoyasema juzi akiwa chuo
kikuu cha Dar es Salaam ili kufanikisha matwaka yao ya kisiasa.
Aidha, Rais Kikwete aliwataka watu hao kumuacha kwani ameshamaliza muda wake wa uongozi hivyo ni wakati wake sasa kupumzika.
Rais
Kikwete pia alikanusha tuhuma za kuwa anatofauti na Rais wa sasa Dkt
John Pombe Magufuli na kusema kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli pamoja
na serikali yake.
Kauli
ya Rais Mstaafu Kikwete ambayo imekuwa ikipotoshwa mtandaoni ni ile
aliyoitoa kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya chuo kikuu cha Dar es
Salaam ambapo aliwataka viongozi wapya kuenzi mazuri ya nyuma
akimaanisha kwamba hivi sasa yeye ndo Mkuu wa Chuo hicho(Chancellor),
hivyo akaahidi kuyaenzi mazuri aliyoyakuta toka kwa watangulizi wake
“Ukiwa mpya lazima watu waone una mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo," alisema Rais Mstaafu Kikwete na kuongeza; “Sio mapya ya kubomoa ya kule tulikotoka,”
No comments:
Post a Comment