Sunday, October 30, 2016

DC NDEJEMBI AZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO)

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
Ofisa Kilimo Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Mumba akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Okoa Njaa Wilayani Kongwa
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Richard Mwite
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi akisisitiza vijana Kulima na kuacha kucheza mchezo wa Pool Table wakati wa kazi

Na Peter Daffi, Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia wananchi kuondokana na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo sambamba na Taifa kwa ujumla.

Kuanzishwa kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa Kata zote zilizopo Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.

Akizindua kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Mwezi Octoba kwa ajili ya msimu wa mwaka 2016/2017 na inatarajiwa kuwa kampeni Endelevu katika kipindi cha Miaka mitano.

Ameeleza kuwa huu ni mkakati maalumu katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ili kukabiliana na hali ya Ukame ambayo ni tatizo sugu katika maeneo mengi nchini.

Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.

Katika kukabiliana na njaa mahitaji mengine mahususi yametajwa ikiwa ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta mwaka 2016 hadi tani3/hekta ifikapo mwezi June 2021, Kuongeza Uzalishaji wa Muhogo mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta mwaka 2029, Kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016 hadi tani 1.8/hekta mwaka 2021.

Pia Mhe Ndejembi alisema kuwa mahitaji mengine ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani 1.2/hekta ifikapo june 2021, pamoja na Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh 500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.

DC Ndejembi ameagiza kufanyika utaratibu wa kuhakikisha kila kaya inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za Mahindi, kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi.

Pia amewaagiza vijana wote wasio na kazi Wilayani Kongwa wapewe Hekari mbili kila mmoja ili waache kucheza pool table na kujihusisha na vikundi Ovu vya wizi na matumizi ya Dawa za kulevya.

Saambamba na hayo Mhe Ndejembi aamepiga marufuku kuchezwa mchezo wa Pool Table mpaka ifikapo majira ya saa 10 jioni, hivyo kwa yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atakuwa amekiuka amri halali ya serikali.

No comments:

Post a Comment