Dar es Salaam Oktoba 28, 2016-
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuanza kwa sherehe
maalumu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti
Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi
upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari,
Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, alisema mbali na kuonesha
mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita,
kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa
Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo
kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.
“Tunawashukuru
wateja wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi,
serikali na wadau wote ambao kimsingi wametusaidia na kuwa nasi
katika safari yetu hii ya mafaniko,” alisema Weesie.
Bia
ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa
asilimia 100hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania
aitwaye Winston Kagusa ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia
za kijerumani na vionjo vya hapa nchinikupata kupata kinwaji hiki
kinacopendwa na wengi.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya
kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii
ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la
mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji
zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza.
Aidha
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha
miongo miwili bia ya Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano
tofauti tofauti vinavyoakisi mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya
wateja wake. “muonekano mpya tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa
kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali mahitaji ya wateja wetu na tuko
karibu nao, amesema Weesie.
“Tunaona
fahari kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager katika ubora uleule
wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi
kutokana na kutambuliwa na wateja wetu wa ndani pamoja na medali
zaidi ya 10 za kutambulika kimataifa ambazo bia hii imeshinda.
Tunaahidi wateja wetu kwamba tutaendeleakuzalisha Serengeti Premium
Lager katika ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia vigezo vya ubora
vilivyoanishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la
Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema Weesie.
Uzinduzi
wa muonekano mpya wa bia ya Serengeti pia umekuja na kauli mbiu mpya
wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” Aidha kampuni
hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za
umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya
Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurungezi
wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari mara baada ya kutangazwa kwa maadhimisho ya miaka 20 tangu
kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka
1996.Anayefuatia katikati ni Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi na
mwishoni kulia ni Mkurungezi mkuu wa SBL Helene Weesie.Mkutano huu
umefanyika mapema jana katika Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.
Mpishi
Mkuu mtanzania Winston Kagusa aliyefanikiwa kuchanganya mbinu ya
utengenezaji wa bia za kijerumani na vionjo vya hapa nchini kupata
kinywaji hiki cha Serengeti Premium Lager kinachopendwa na wengi.
Mkurugenzi
Mkuu wa SBL Helene Weesie akiongoza katika kuzindua chapa mpya ya
Serengeti Premium Lager sherehe ambazo zinaambatana na maadhimisho ya
miaka 20 ya bia hiyo kulia kwake ni Meneja Masoko wa SBL Anitha na
kushoto kwake wa kwanza ni Mpishi Mkuu wa kwanza wa Serengeti Premium
Lager Winston kagusa na mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko Cesear
Mloka.Hafla hii ilifanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano, SBL John Wanyacha akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari katika Mkutano wa waandishi wa habari ambapo Bia ya serengeti
premium lager inatimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake na pia
kuzinduliwa kwa chapa yenye muonekano mpya.Mkutano huu ulifanyika mapema jana katika hotel ya Hyatt Regency
No comments:
Post a Comment