Na Daudi Manongi-MAELEZO
Kampuni
ya Ndege Tanzania (ATCL) imetoa ofa ya mwezi mmoja kwa abira
wanaosafiri kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza kulipa nauli ya shilingi
160,000/- kwa safari moja.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na na Kaimu Afisa Mawasiliano
wa Kampuni Bi.Lily Fungamtama wakati akiongea na Idara ya Habari.
Amesema
Ndege za Kampuni zimeanza kutoa huduma kuanzia Jumamosi ya wiki
iliyopita ya tarehe 15 ya mwezi huu kama ilivyobainisha kupitia vyombo
vya Habari.
Safari
hizo zilianza kwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kuelekea nchini
Comoro na hapa nchini itoa safari katika mikoa ya Mwanza, Arusha na
Kigoma.
Bi.Fungamtama
amesema kwa kuanzia walianza na mazoezi ya vitendo kwa marubani na
wafanyakazi wa ndani ya Ndege ambapo hatimaye walianza safari za
biashara ya kusafirisha abiria mnamo tarehe 15 Oktoba kama ilivyopangwa.
Ameongeza
kuwa ATCL imeboresha huduma zake kwa kiasi kikubwa kwa kuwapatia wateja
wake ofa ya kubeba kilo 20 za mizigo na kilo 7 za mzigo wa mkononi
bure pamoja na kutoa vinywaji na ubadilishaji wa tiketi ni bure ndani
ya mwezi.
Aidha, Kaimu Afisa Mawasiliano wa Kampuni Bi.Lily amekanusha taarifa potofu kuwa zimekwama kuanza safari zilizopangwa.
Amesema kuwa habari hizo sio za kweli kwani hivi sasa wameshaanza huduma katika mikoa hiyo mitatu.
Kampuni
ya Ndege ya ATCL kwa sasa ina ndege tatu,zikiwemo mbili aina ya
Dash8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na Dash8-Q300 moja
yenye uwezo wa kubeba abiria 50.
No comments:
Post a Comment