Meneja
Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari
kusiana na huduma mpya ya linda simu ya Airtel Simu Bima itakayowasaidia
wateja wote wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na
kulipia kupitia huduma ya Airtel Money, kulia ni Meneja wa Airtel Money
Bw, Moses Alphonce na kushoto ni Muwakilishi wa shirika la Bima la UAP
bw, Charles Matondane
Toka
kulia ni meneja wa Airtel Money bw, Moses Alphonce akiwa na Meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakionyesha jinsi huduma yao ya
kulipia simu za smartphone Bima ijulikanayo kama “Linda simu na Airtel
Simu Bima” Inavyofanya kazi. Kupitia huduma hiyo sasa wateja wote
wanaotumia Smarphone nchni wataweza kuziwekea Bima zao simu kulipia
kupitia huduma ya Airtel Money na endapo simu hiyo itaibwa au kupotea
mteja atalipwa ndani ya siku tano. kushoto anaefuatilia uzinduzi huo ni
muwakilishi wa kampuni ya bima ya UAP Tanzaninia bw Charles Matondane
ambao wao watakuwa wakiwalipa wateja.
Meneja
Masoko wa kampuni ya Bima ya UAP bw, Raymond Komanga akielezea jinsi
mfumo wa malipo wa Airtel SimuBima unavyofanya kazi kwa kushirikiana
kampuni yake mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo ya kulinda simu za
smartphone kupitia bima ijulikanayo kama Airtel SimuBima, katikati ni
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na Meneja wa Airtel Money bw,
Moses Alphonce (kulia) huduma ya AirtelSimuBima itawawezesha wateja wa
Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale
simu inapopotea au kuibiwa.
·Wateja wa mitandao mingine pia wataweza kusajili simu zao na bima hiyo na kulipia kwa Airtel money
·Airtel Simu Bima kufidia simu za wateja wake zilizopotea au kuibwa
Kampuni
ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya UAP leo
wamezindua huduma kabambe itakayowasaidia wateja wote wanaotumia Simu
za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya
Airtel Money.
Huduma
hiyo mpya nchini kwa watumiaji wa smartphone itajulikana kama “Airtel
SimuBima” ambapo itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote
wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.
Akiongea
wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson
Mmbandoalisema “Leo Airtel tumeongeza sababu nyingine kwa wateja wetu
kuendelea kufurahia huduma zetu, sasa wateja wote wenye simu orijino za
smartphone wataweza kusajiliwa na huduma ya ‘Airtel
SimuBima’ ambapo mteja mmoja anataweza kusajili hadi simu mbili katika
mfumo huu. Ikitokea mteja ameibiwa simu yake au kuipoteza basi kupitia
huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ tutampatia mteja huyo pesa ili aweze
kununua simu nyingine atakayotaka na kisha simu iliyopotea itazimwa moja
kwa moja isiweze kutumika tena”.
“Mteja wa
Airtel ataweza kufaidi huduma ya “Airtel SimuBima” mara baada ya
kupakuwa aplikesheni ya simuBima kutoka kwenye Playstore na kusajili
taarifa za smartphone yake ikiwemo IMEI namba pamoja na gharama ya simu
yake na papohapo atapata ujumbe utakaomwambia gharama ya Bima ya simu
hiyo kwa mwaka ambayo ataamua kuilipa yote au kuwa anailipa kwa kila
mwezi” aliongeza Mmbando
“Airtel
Tanzania tunaamini kuwa ushirika wetu na shirika la bima la UAP
kupitia ‘Airtel SimuBima’utasaidia kuhamasisha watumiaji wa simu za
mkononi kununua simu orijino ili waweze kufurahia huduma hii pamoja na
huduma zingine za Airtel za kimtandao kama vile Airtel TV, Kujisomea
masomo ya VETA –VSOMO kupitia mtandao pamoja na kufaidi aplikesheni
mbalimbali za airtel zenye kusaidia wateja katika mambo ya kiuchumi na
kijamii” alieleza Mmbando
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa UAP Bw, Raymond Komanga alisema
“tunawahakikishia wateja wote wa Airtel watakaosajili namba zao katika
huduma ya Airtel SimuBima kwamba tutawalipa madai yao haraka sana pale
wanapopatwa na tatizo la kupoteza simu au kuibiwa simu zilizowekewa Bima
ndani ya siku tano tu tokea pale wanapotoa taarifa kituo cha polisi na
kutujulisha sisi, tutalipa simu za hadi shilingi milioni moja na laki
tano, lakini wateja waelewe kuwa bima yetu haitakuwa ikilipa simu
kuvunjika au
Komanga
aliendelea kuelezea kuwa “Ikitokea simu ya mteja iliyosajiliwa
na “Airtel SimuBima”imepotea au kuibiwa mteja atatakiwa kutoa taarifa
mapema sana na kupata taarifa ya polisi kuhusiana na upotevu huo au wizi
ili kuweza kukamilisha malipo yake. Swala hili linatakiwa kufanywa na
wateja wote waliojisali na kulipia bima ya mwezi au ya mwaka mzima
kupitia Airtel SimuBima”
Wateja wa
“Airtel SimuBima” wataweza kudai malipo yao kwa kutumia simu nyingine
ya smartphone na kuingia katika Aplikesheni ya Airtel SimuBima kisha
kufuata maelekezo ya malipo. Vilevile mteja anaweza kutumia kompyuta na
kuingia katika ukurasa wa ‘Airtel SimuBima’ na kukamilisha taarifa za
madai.
No comments:
Post a Comment