September
10 2016 lilitokea tetemeko la ardhi Kagera kanda ya ziwa Tanzania lenye
kipimo cha 5.7 na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine zaidi ya 100
kujeruhiwa ambapo ndani ya saa 24 baadae (September 11 saa tano kasoro
usiku) likatokea tena tetemeko jingine.
Tetemeko
hilo la pili ambalo ni dogo halijaripotiwa kusababisha majeruhi au vifo
mpaka usiku wa saa nane lakini limeleta hofu kwa wakazi wa Bukoba ambao
baadhi wameamua kutoa magodoro nje ya nyumba zao na kulala kwa kuhofia
tetemeko linaweza kutokea tena usiku na kuwakuta ndani ya nyumba zao.
No comments:
Post a Comment