Wakala
ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekusudia kuendesha kampeni maalum ya
kupima matumizi ya vilevi kwa madereva wanaosafirisha abiria na mizigo
ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani nchini.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa
Samwel Manyele alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wadau wa
kemikali juu ya matumizi salama ya kemikali nchini.
Profesa
Manyele alisema utaratibu wa kuwapima madereva hao utaanza hivi
karibuni na utawezesha kupunguza tatizo la ajali barabarani na kuvitaka
vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.
“Madereva
wote wanaosafirisha mizigo na abiria watatakiwa kupita kwenye kipimo
ambacho kitaonyesha kama madereva hao wanatumia vilevi, hali hiyo
itasaidia kutatua tatizo la ajali za barabarani nchini”, alisema Manyele.
Profesa
Manyele alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutoa uwezo na uelewa kwa
wahusika hasa wasimamizi wa shughuli za kemikali na matumizi salama
juu ya kukabiliana na matukio au ajali za kemikali pale yanapotokea.
No comments:
Post a Comment