Na Mathias Canal, Singida
Waislamu duniani kote leo wanasherehekea sikukuu ya Idd El Hajj
wakiungana na wale (Mahujaji) walioko katika miji ya Makkah na Madina,
nchini Saudi Arabia wakiendesha ibada mbalimbali.
Barani Afrika
sikukuu hii inasherehekewa katika nchi mbalimbali, huku baadhi ya nchi
zikiwa katika hali ya sintofahamu kutokana na makundi yanayodai kuwa
yenye msimamo mkali wa kidini, hasa nchini Somalia, Nigeria, Mali,
Libya, Mauritania na nchi nyingine za Kiarabu barani Asia, na Ulaya.
Nchini Tanzania sala ya Idd El Hajj imeswaliwa Katika viwanja vya
BAKWATA Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam huku Mufti Mkuu wa
Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally pamoja na viongozi wakuu
wakishiriki sala hiyo.
Wilayani Ikungi Mkoani Singida waumini wa
Dini ya Kiislamu wametakiwa kushirikiana kwa pamoja na waumini wa dini
zingine ili kuongeza ufanisi wa amani na chachu ya maendeleo nchini
Tanzania katika nyanja zote ikiwemo kuboresha huduma ya elimu, afya na
Miundombinu.
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
ameyasema hayo hii leo wakati akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu
katika msikiti wa Masjid Noor uliopo katika Kijiji cha Makiungu
nakuwataka waumini hao kujitokeza kwa wingi katika kukamilisha ufanisi
wa utendaji kazi ili kuimudu kasi ya serikali ya awamu ya nne chini ya
Rais John Pombe Magufuli ya HapaKaziTu.
Kati ya Waislamu duniani
sikukuu hii hujulikana kwa majina mbalimbali ambayo hutafsiriwa pia kwa
lugha mbalimbali kama vile: Idd-al-Adhha yaani sikukuu ya sadaka,
Idd-al-Qorban sikukuu ya sadaka (kwa kutumia neno tofauti ya "sadaka"
katika Qurani); Kituruki: Kurban Bayramı; Kikurdi "Cejna Kûrbanê" ;
Idd-al-Kabir au "sikukuu kubwa"; "Bari Eid" huko Uhindi na Pakistan;
jina hili hutumiwa kwa sababu kati ya sikukuu mbili zinazoamriwa katika
Qurani hii ni sikukuu kubwa zaidi.
Mtaturu alisema kuwa Wilaya ya
Ikungi imecheleweshwa na utengano wa Itikadi za Kisiasa hadi kufikia
hatua ya wananchi kuacha kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi
wa maabara
Katika sikukuu ya Idd Kila Mwislamu mwenye uwezo
hupaswa kumchinja mnyama wa sadaka siku hiyo mara nyingi kondoo lakini
kuna pia sadaka za mbuzi, ng'ombe au ngamia kufuatana na uwezo na
kawaida ya nchi.Sehemu ya nyama ya sadaka hizo hugawiwa kwa maskini
wasio na uwezo na Mengine hutumiwa kwa karamu ya familia.
Dc
Mtaturu amesema kuwa kwa umoja wa wazawa na wakazi wasio wazawa katika
Wilaya hiyo utaimarisha na kuongeza weledi na kukuza kipato cha kila
mmoja kwa kuongeza juhudi za utendaji kazi.
Idd husheherekewa
kati ya tarehe 10 hadi 13 ya mwezi wa Dhul Hijjah wa kalenda ya
Kiislamu. Tarehe hali halisi hutegemea na kuonekana kwa hilali au mwezi
mwandamu. Hapa hutokea tofauti za kila mwaka kati ya Waislamu. Kimsingi
mapokeo ya kiislamu hudai kuonekana kwa mwezi kwa macho.
Kubadilika kwa tarehe katika kalenda ya jua
Katika kalenda ya Gregori ambayo ni kalenda ya kawaida tarehe za Kiislamu hubadilika kila mara kwa sababu mwaka wa kiislamu hufuata kalenda ya mwezi lakini kalenda ya kawaida hufuata jua.
Kalenda
ya Kiislamu ni takriban siku 11 kasoro ya kalenda ya jua. Kila mwaka
tarehe ya Idd huweza kutokea kwa siku mbili tofauti za kalenda ya
Gregori kwa sababu kawaida ya Uislamu hufuata kuonekana kwa mwezi
kunachopatikana tofauti duniani.
No comments:
Post a Comment