Leo Septemba 10, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Miongoni
mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa
kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia
jumatatu hadi Ijumaa.
Hudson
Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Hii
sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji kushika
nyadhifa mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin
Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Wakurugenzi wengine walioteuliwa leo ni pamoja na;-
- Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
- Godfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
- Yusuf Daudi Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
- Bakari Kasinyo Mohamed – Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
- Juma Ally Mnwele – Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
- Butamo Nuru Ndalahwa – Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
- Waziri Mourice – Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
- Fatma Omar Latu – Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
- Godwin Emmanuel Kunambi – Manispaa ya Dodoma
- Elias R. Ntiruhungwa – Mji wa Tarime
- Mwantumu Dau – Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
- Frank Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
No comments:
Post a Comment