Sunday, September 11, 2016

KESHO NI SIKU YA IDI TAMBUA MAMBO MUHIMU JUU YA IDI



Neno la Wakati Mwema

Siku ya iddi ni siku ya furaha Na iddi ni alama miongoni mwa alama kubwa za dini.Katika dini yetu ya kiislamu tuna iddi mbili Iddi el fitri(iddi ndogo) na Iddi el adh-haa(iddi kubwa) Kesho siku ya jumatatu ni tarehe kumi ya mwezi wa dhul hijja mwaka 1437. Na ndio siku ya iddi el adh-haa,itakayokuwa ikiafikiana na tarehe 12/9/2016.
Ni sunna kuchinnja ndani ya iddi hii. Na wanyama wa kuchinjwa ni ngamia,ng`ombe mbuzi na kondoo. Ngamia na ng`ombe yajuzu kushirikiana watu saba, Ama mbuzi na kondoo ni kwa mtu mmoja tu. Pia mnyama huyu mwenye kuchichwa haitakiwa awe na aibu,kama kilema,kipofu au maradhi.

Ni vizuri nyama ukaigawa katika mafungu matatu:

1:Familia yako
2:Mafakiri na masikini

3:Majirani na marafiki

Muda wa kuchinja ni baada ya swala ya iddi,ama kwa yule Atakaye chinja kabla ya swala basi haitohesabika kama umetekeleza ibada hii ya kuchinja.Pia mtu anaweza chinja siku hiyo ya iddi,siku ya pili na siku ya tatu.

Ni sunna kuswaliwa swala ya iddi uwanjani.Yapendeza vile vile watu wote kuelekea katika swala ya iddi Wakiwemo wanawake hata walio katika siku zao.Iwapo kama swala hii itaswaliwa msikitini basi wanawake hao walio katika siku zao watakaa karibu  na msikiti na wala si kuingia msikitini.

Ni sunna kuoga ndani ya siku hii, na muda wa kuoga mtu anaweza oga kabla ya swala ya alfajiri
au baada ya swala ya alfajiri. Muda wa swala ya iddi ni toka baada ya kuchomoza kwa jua na kurefuka kiasi mpaka kugeuka kwa jua. Ni vizuri kuwahishwa swala ya iddi el adh-haa na kucheleweshwa swala ya iddi el fitri.

Hekima juu ya hili ni kwamba: Katika iddi el adh-ha ni sunna kuelekea katika swala Hali ya kuwa hujala chochote(umefunga) Ama katika iddi el fitri ni sunna kufuturu kwanza kabla
ya kwenda kuswali,kwa hiyo huenda iwapo kama katika iddi  el adh-haa swala itacheleweshwa huenda ikawakera baadhi ya watu na kusumbuliwa na njaa.Ni sunna katika siku ya iddi kuvaa nguo nzuri Na ni bora rangi ya nguo ikawa ni nyeupe. Kama mtu atakuwa na nguo aina mbili moja ni nyeupe Na nyingine ni rangi tofauti na nyeupe,iwapo kama ile nguo ambayo si nyeupe itakuwa ni nzuri kuliko nyeupe basi aivae  hiyo isiyokuwa nyeupe.

NB:Mavazi yanayo takiwa kuvaliwa yawe ni yale mavazi yanayo kubaliwa na sheria ya dini yetu tukufu ya kiislamu.

Ni sunna wakati wa kwenda kuswali kupita njia na wakati wa kurudi kupita njia nyingine tofauti na ile ya mwanzo. Swala ya iddi haina swala za sunna kabla ya swala Baada ya kurudi nyumbani waweza swali rakaa mbili.Swala ya iddi haina adhana wala iqaama na wala hainadiwi Asswalaatu jaamia.

Idadi ya takbira(Allahu akbaru) katika swala ya iddi ni takbira saba katika rakaa ya kwanza ikiwemo takbiratul ihram (takbira ya kuhilimia swala),na katika rakaa ya pili ni takbira tano
pasina ya kuhesabu takbira ya kutoka katika sijda. Na kuna wanazuoni wanao ona ya kwamba idadi ya takbira za rakaa ya kwanza ni saba pasina ya takbira ya kuhilimia, lakini dalili yake ni dhaifu.Takbira katika iddi hii huanza alfajiri ya siku ya arafa na huendelea mpaka siku ya tatu baada ya siku ya iddi. Sikuu ya iddi ni siku ya utiifu pia Kwa hiyo ni juu yetu kufurahi kama vile uridhiavyo uislamu

Anasema mtume wetu Muhamadi-rehema na amani ziwe juu yake- (Mwenye kumuasi Allah siku ya iddi ni kama vile kamuasi siku ya kiyama) Siku ya kiyama ni siku yenye kutisha siku ambayo Kila mmoja wetu atakutana na yale aliyo yatanguliza. Kafiri atatamani awe mchanga,sasa itakuwa ni suala  La kushangaza sana iwapo kama mmja ataendelea kumuasi Mwenyezi Mungu ndani ya siku hii.

No comments:

Post a Comment