Clinton aliishiwa nguvu wakati wa kumbukumbu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11
Mgombea
Urais kupitia Chama cha Democratic nchini Marekani Bi Hillary Clinton
amerejea kwenye mbio za kampeni baada ya kuugua homa ya mapafu.
Akiongea
na mwandishi wa habari akiwa kwenye ndege kuelekea Greensboro North
Carolina, Bi Clinton alisema anajiskia vizuri baada ya mapumziko ya siku
tatu.
Mpinzani wake wa Chama cha Republican, Donald Trump ametoa barua kutoka kwa daktari wake ikionesha kuwa ana afya njema.
Barua
hiyo inaonesha kuwa anatumia dawa ili kupunguza unene na kiwango
kilichopitiliza cha uzito, lakini hatumii kilevi wala kuvuta sigara.
Trump aliwahi kuwa mchekeshaji wa vipindi vya runinga
Uchaguzi
wa Marekani utafanyika mwezi Novemba ambapo kampeni zake zimekuwa na
vuta ni kuvute kutoka vyama vikubwa viwili vya Democratic na Republican. BBC
No comments:
Post a Comment