NA HASSAN SILAYO-MAELEZO,KAGERA
Benki ya
FINCA Microfinance imewasamehe mikopo yenye thamani ya shilingi milioni
57.2 wateja wake 15 waliothibitishwa kuathirika kwa tetemeko la ardhi
lililotokea terehe 10 mwezi huu mkoani Kagera.
Hayo
yamesemwa na Meneja wa Kanda wa FINCA Bw. Aluto Hagamu wakati
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu
misaada kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani humo.
Bw.
Hagamu alisema kuwa dhumuni kubwa la benki hiyo la kufuta mikopo hiyo ni
kuwapunguzia mzigo wanachama hao kutokana na athari walizozipata
kutokana na tetemeko hilo na kuwawezesha kurudi katika shughuli
wanazozifanya ili kujiweka sawa kiuchumi.
Aidha,
Bw. Hagamu kwa niaba ya benki hiyo pia wamekabidhi Sukari mifuko 25,
mabati bando 5 pamoja na misumari katoni 8 kwa dhumuni kusaidia waathika
wa tetemeko hilo.
No comments:
Post a Comment