Monday, August 15, 2016

WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI YASAINI HATI YA MAKUBALIANO NA TANZANIA WATER PARTNERSHIP

den01
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba na Mtendaji Mkuu wa Tanzania Water Partnership, Dkt. Victor Kongo wakibadilishana Hati za Makubaliano ya Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini mara baada ya kutia saini.
den1
Wajumbe walioshiriki katika kikao cha kutia saini Hati ya Makubaliano ya Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini kati ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Tanzania Water Partnership.
den2
Meneja Mipango, Andrew Takawira (kushoto) na Afisa Mipango, Michael Raamano kutoka Taasisi ya Global Water Partnership ya Afrika ya Kusini walikuwa ni miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho.
den3
Mtendaji Mkuu wa Tanzania Water Partnership, Dkt. Victor Kongo akizungumza, kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Hamza Sadiki na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba.

den4
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba akiwa pamoja na Wakurugenzi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, wajumbe wa Global Water Partnership na Tanzania Water Partnership mara baada ya kikao cha kusaini Hati za Makubaliano ya Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji leo imesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati yake na Shirika lisilo la Serikali, Tanzania Water Partnership (TWP) kwa ajili ya utekelezaji wa Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini.

Makubaliano hayo yalisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba na Mtendaji Mkuu wa Tanzania Water Partnership, Dkt. Victor Kongo na kuhudhuriwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na wajumbe kutoka Tanzania Water Partnership.

Lengo kuu la ushirikiano huo likiwa ni kutunza na kusimamia rasilimali za maji nchini kwa ajili ya maendeleo endelevu ya upatikanaji wa maji nchini na kuinua kiwango cha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi wote Tanzania.

No comments:

Post a Comment