WAZIRI
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amewanyooshea kidole
maofisa ugani wa mifugo na uvuvi kwa maelezo kuwa wameacha kutimiza
majukumu yao na badala yake wanakamata zana haramu za uvuvi, kuuza dawa
na kuomba hongo.
Dk
Tizeba alisema hayo juzi alipotembelea maonesho ya kitaifa ya mifugo
katika viwanja vya maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika
Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kanda ya Kati Nzuguni mjini Dodoma.
Alisema
maofisa ugani upande wa kilimo, ufugaji na uvuvi hawawajibiki ipasavyo
na wamejibadilisha kuwa wafuatiliaji na wakamataji wa zana haramu za
uvuvi, kuuza dawa za mifugo na kupokea hongo.
Pia alisema maofisa nyama wamebaki kuchukua baadhi ya nyama kama hongo na kuruhusu nyama kuuzwa bila kukaguliwa kitaalamu.
Alimuagiza
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mary Mashingo kufuatilia utendaji kazi
wa Baraza la Usajili wa Maofisa Ugani hao, huku akimtaka pia mwenyekiti
wake wa bodi hiyo kumpatia mpango kazi walionao na changamoto zilizopo
katika kuwasimamia ili wawajibike vyema zaidi.
Dk
Tizeba alisema baraza hilo, mwenyekiti wake wa bodi kuhakikisha kuwa
anatengeneza mfumo utakaotoa vibali vya muda utakaowezesha bodi yake
kuwapima utendaji wao kwanza kabla ya kuwapatia usajili wa kudumu.
Pia
alimuagiza katibu mkuu kutoa maagizo kwa halmashauri zote nchini ili
maofisa ugani hao wanapotekeleza wajibu wao chini ya usimamizi wa
wakurugenzi wao wawe na mfumo ulio wazi na wenye tija katika kuwahudumia
walengwa vizuri zaidi na si kama wanavyofanya sasa kwani hawawajibiki
na hawasimamiwi ipasavyo.
Ofisa
Mifugo wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Gracian Mwesiga alisema inawezekana
kuwepo kwa maofisa mifugo wasiotimiza majukumu yao, lakini kwa mwenendo
wa sasa wa serikali wanatakiwa kupendekeza na kupitisha sheria
itakayompa meno mwenyekiti wa bodi ya usajili wa maofisa ugani ikiwamo
kufuatilia utendaji wao baada ya kuwasajili.
“Usimamizi wa maofisa mifugo upo kwenye halmashauri na si katika baraza ambalo kazi yake ni kusajili wataalamu,” alisema Mwesiga.
No comments:
Post a Comment