Tuesday, August 16, 2016

Waziri Mkuu wa DRC azuru Beni

media
Jumla ya watu 51 waliuawa katika usiku wa Jumamosi 13 kuamkia Jumapili Agosti 14 nje ya jiji la Beni.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, watu wanaendelea kukimbia eneo lililo karibu na mji wa Beni. Usiku wa Jumamosi 13 kuamkia Jumapili, Agosti 14, kwa mujibu wa asasi za kiraia, watu 51 waliuawa, wengi kwa visu. mauaji haya yalihusishwa waasi wa Uganda wa ADF.

Baada ya kiongozi namba mbili wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) Jumatatu wiki hii, ujumbe wa serikali umewasili Jumanne hii asubuhi katika mji wa Beni. Ujumbe huo ukiongozwa na Waziri Mkuu umezuru eneo la Rwangoma, katika kichaka, ambapo kulitiokea moja ya mauaji.

Kulikuwa na Waziri Mkuu wa DRC Augustin Matata Ponyo, Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani na Usalama, Evariste Boshab. Baraza lote la Ulinzi limzuru maeneo mbalimbali ya mauaji ya mwishoni mwa wiki iliyopita. Ziara iliyofanywa kwa usafiri wa gari, lakini pia viongozi hao walitembea kwa mguu katika kichaka katika eneo la Rwangoma, Mbelu ambapo piakulitokea mauaji.

Ujumbe huu ulikua umezungukwa na idadi kubwa ya vikosi vya usalama na kuongozwa na Mkuu wa mji wa Beni.

Mkuu wa mji wa Beni alieleza kuwa hapa watu watano waliuawa - walikuwa walifungwa kamba, huku nyumba moja ikichomwa moto- baadhi ya watu waliuawa na wengine walijeruhiwa au walinusurika. Ujumbe ulikuwa na mtazamo wa kile kilichotokea, na hilo ndio lengo la ziara iliyoagizwa na rais wa Jamhuri, hivyo ndivyo alivyosema Waziri Mkuu Augustin Matata Ponyo.

Ziara ya kufanya tathmini ya hali iliyotokea na kujaribu kuelewa kile kilichotokea katika nje kidogo ya mji wa Beni.

Hatua za kipekee zaahidiwa

Pia kulikuwa na majadiliano mengi kuhusu kama kulikuwa na ulaji njama. majibu meengi pia yaliyotolewa na Mkuu wa mji wa Beni.

Ujumbe wa Waziri Mkuu wa Congo, Augustin Matata Ponyo, J"Hapana ilikuwa njia ya kawaida inayotumiwa na wasi waADF-Nalu kati ya ngome yao ya Mwalika na 'eneo hili la mauaji' "Jumanne hii asubuhi katika mji wa Beni ulikuwa kwanza kusema kuwa kitendo hiki kiliyotokea ni cha kigaidi.

Waziri Mkuu pia amesisitiza kuwa alitumwa, yeye pamoja na Baraza la Ulinzi, na rais wa jamhuri, ambaye hakuweza kuzuru mji wa Beni, na kwamba watajaribu kujadili uwezekano wa kukabiliana na hali hii ya kipekee kwa sheria za kipekee, ambazo zitachukuliwa hivi karibuni, baada tu ya tathmini hiyo kuwasilishwa kwa Rais Joseph Kabila. 

RFI

No comments:

Post a Comment