Tuesday, August 16, 2016

Trump aeleza mpango wa kupambana na ugaidi

Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump
Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump

Donald Trump ameeleza mpango wake wa kuifanya Marekani kuwa sehemu salama kwa kupambana na kile alichokiita kuwa ni ugaidi wa waislamu wenye itikadi kali. Amesema kama atachaguliwa kuwa rais wa marekani atabadilisha sera za mamabo ya nje za nchi hiyo zenye lengo la kujenga taifa kwa kuwa na sera zenye uhalisia.

Akihutubia mkutano wake katika jimbo la Ohio, mgombea urais kupitia chama cha Republican alisistiza juu ya umuhimu wa mpango wa muda wa kuzuia viza za waombaji wanaotoka katika nchi ambazo zina historia ya kueneza ugaidi ,na kupendekeza kuanzishwa kwa
mifumo ya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa akauti zao za mitandao ya kijamii.

Aidha bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na nchi yoyote ile bila kujali tofauti za kiitikadi au mikakati akiwa na nia ya kusaidia kulitokomeza kundi la Islamic State. 

BBC

No comments:

Post a Comment