Kikosi
cha timu ya Serengeti Boys kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya
mchezo wa timu hizo ulichezwa katika uwanja wa Dobsonville ulioko
Soweto, Mji ulioko Kusini –Magharibi mwa jiji la Johannesburg nchini
Afrika ya Kusini
Ibrahim
Abdallah wa Serengeti Boys akibanwa na Beki wa Amajimbos, Sechala
Makoena wakati wa mchezo huo uiochezwa katika uwanja wa Dobsonville
ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini –Magharibi mwa jiji la Johannesburg
nchini Afrika ya Kusini
Naibu
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Rosemary Jairo (wa pili
kushoto) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wakiwa wamezungukwa na nyota wa
Serengeti Boys.
Ikicheza
mbele ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi na Naibu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Rosemary
Chambe Jairo, timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
maarufu kama Serengeti Boys leo imegoma kupoteza mchezo dhidi ya wenyeji
Afrika Kusini baada ya kuibana Amajimbos na kutoka sare bya bao 1-1.
Katika
mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko
Kusini –Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana
kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti kwa kila upande. Afrika Kusini
walianza kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa na Linamandlia
Mchilizeli kabla ya Ally Msingi kuisawazishia Serengeti Boys katika
dakika ya 70.
Penalti
ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys
kumfanyia madhambi Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya eneo la hatari
wakati ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos
kunawa mpira eneo la hatari.
Afrika
Kusini iliyoanza kwa kasi dakika 10 za mwanzo wa mchezo huo, ilipotea
dakika zote 30 za kipindi cha kwanza ambao kukosa bahati na umakini
kidogo tu kwa nyota wa Serengeti Boys kulisababisha kukosa mabao matano
yakiwamo mawili yaliyogonga mwamba hivyo kuwatia hasira Serengeti Boys
ambao walionyesha kuwa na njaa ya mabao.
Kubanwa
katika kipindi cha kwanza, kulisababisha Kocha Mkuu wa Amajimbos kufanya
mabadiliko ya wachezaji wote watatu kipindi cha pili, wakati Bakari
Shime kwa upande wake alimpumzisha Ibrahim na nafasi yake kuchukuliwa na
Muhsin ambaye alisaidia kuendedlea kuwabana Afrika Kusini waliokjuwa
wanawategemea nyota kama na Mswati Mavuso na Lethabo Mazibuko.
Shukrani
za pekee zinaweza kwenda kwa Kipa Ramadhani Kabwili aliyeokoa hatari
nyingi ikiwamo mpira uliokuwa unakwenda golini uliotokana na adhabu
ndogo. Kadhalika Msengi aliyekuwa nyota wa mchezo huo akimiliki vema
idarta ya ulinzi akishirikiaana nDickson Job.
Shime
maarufu kama Mchawi Mweusi alisema: “Nashukuru kwa matokeo haya. Si
mabaya kwangu. Tunarudi nyumbani kujipanga. Afrika Kusini ilikuwa
inanitia hofu ndio maana nilisema mechi itakuwa ngumu.”
Kwa
upande wake, Naibu Balozi Rosemary alisema: “Ahsanteni vijana (Serengeti
Boys) kwa kulinda heshima yangu,” wakati Malinzi alisema: “Sina mengi.
Mkiwafunga Afrika Kusini Agosti 21, 2016 kambi inapigwa tena nje ya
nchi. Sijui ni nchi gani, lakini mtakwenda kujiandaa nje ya nchi.”
Katika
mchezo huo, Kikosi cha Serengeti kilikuwa: Ramadhani Kbawili, Israel
Mwenda, Nickson Kibabage, Ally Msengi, Dickson Job, Shaban Ada, Kelvin
Naftal, Ally Ng’anzi, Ibrahim Abdallah/Muhsin Makame (Dakika ya 72),
Asad Juma na Mohammed Rashid.
No comments:
Post a Comment