Na Abushehe Nondo na Sheila Simba-Maelezo
Serikali
imesema kuwa iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier
Q400 kutoka nchini Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa
anga kwa safari za ndani ya nchi na mazingira halisi ya viwanja vya
ndege vilivyopo nchini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
wakufunzi wa marubani katika chuo cha Taifa cha usafirishaji(NIT)
Mbarawa
alisema kuwa Serikali haikukurupuka katika kufanya maamuzi ya aina ya
ndege za kununua badala yake imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya
kuhudumia usafiri wa ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika
la Ndege Tanzania (ATCL).
“Serikali
imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali
halisi ya Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa
baadhi, huku lengo ni kutoa huduma za usafiri wa ndani” Alisema Profesa
Mbarawa.
Mbarawa
aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni kuhudumia wananchi
hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani zimezingatia mambo
mbalimbali ikiwemo suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.
Aliongeza
kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua katika viwanja vingi hapa nchini
kwani zinaweza kutua katika viwanja vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo
ndio vingi nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja
vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.
Prof.
Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza uwezo mdogo wa
ndege hizo katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina zingine ambapo
kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa zikitumia Tani
1.7 za mafuta tofauti na aina nyingine zinazotumia hadi Tani 2.8 kwa
safari moja.
Waziri
Mbarawa pia alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege
hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha
kuwa suala hilo siyo la kweli kwani kampuni hiyo imefanya biashara na
nchini nyingi ikiwemo Ethiopia yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400
zilizotengezwa na Kampuni hiyo.
Mpaka
sasa tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa
asilimia 40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchi tarehe 19
septemba mwaka huu ambapo zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe
15 septemba mwaka huu kupitia nchini Uingereza.
Akizindua
mafunzo hayo ya wakufunzi wa marubani, Waziri Mbarawa aliwaasa
Marubani ambao watahitimu mafunzo hayo kuhakikisha wanazingatia suala
na nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya usafiri wa anga.
“Hatutaki
kuwa na marubani ambao wana uwezo wa kazi lakini sio
waadilifu,hakikisheni mnawafundisha marubani wanafunzi kuzingatia
nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya anga ambapo wakati mwingine
Rubani anajijua anakasoro lakini bado anang’ang’ania kurusha ndege”
alisema Prof.Mbarawa.
Aidha
amesema kuwa Serikali itashirikiana na chuo hicho katika kutoa kozi za
urubani ili kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa marubani nchini.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendesha
ndege kwa kutumia kifaa maalum cha kufundishia marubani (simulator)
kwenye chumba cha mafunzo kwenye Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Mkuu
wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa
akizungumza na wadau wa sekta ya usafiri wa anga (hawapo pichani) katika
uzinduzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani uliofanyika jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua
jambo kwa wadau wa sekta ya usafiri wa anga (hawapo pichani) katika
uzinduzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani uliofanyika jijini Dar es
salaam.
Wadau
wa sekta ya usafiri wa anga wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika uzinduzi wa mafunzo ya
wakufunzi wa marubani uliofanyika jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment