Ofisi
za Bunge zilizopo Jijini Dar es salaam zinatarajia kuhamishiwa Dodoma
mwezi Septemba mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa agiza la Rais Magufuli
la kuhamishia shughuli za serikali Dodoma.
Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai jana na kusema kuwa kwa bunge suala la luhamia Dodoma siyo gumu kwa kuwa tayari makao makuu yake yako Dodoma.
Alisema
tayari alikwishatoa maagizo kwa ofisi yake kuhakikisha kuwa kufikia
mwezi Septemba kila kitu kinachofanyika Dar es salaam kifanyike Dodoma
isipokuwa mambo machache.
"Nimeagiza
ofisi yangu ihamie dodoma mara moja kuanzia Septemba hii, watumishi wa
bunge karibu wote watahamia Dodoma, masuala ya malipo yataangaliwa
baadaye, kwa sasa ni kuhamia dodoma tu, ofisi tunazo huko" Alisema Ndugai
Kama
sehemu ya mwanzo wa utekelezaji wa azma hiyo, tayari ofisi ya bunge
imetangaza kufanyia Dodoma vikao vyake vyote vya kamati za bunge tofauti
na ilivyokuwa umepangwa mwanzo na ilivyozoeleka kufanyikia Dar es
salaam.
No comments:
Post a Comment