Kaimu
Mkurugenzi wa Urasimishaji makazi holela toka Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Bibi Betha Mlonda akifafanua kwa waandishi wa Habari
kuhusu mpango wa urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholea katika Jiji
la Dar es saaam ambao umeanza kutekelzwa katika eneo la Kimara Jijini
humo .kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari- Maelezo Bi Fatma Salum
na kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Hassan Mabuye.
Baadhi ya
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi na Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es salaam.
Moja ya eneo lenye makazi holela katika Jiji la Dar es salaam.
Mmoja wa Wataalamu wa upimaji Ardhi akiweka alama katika eneo lililorasimishwa.
Fatma Salum-Maelezo
Serikali
imeanza kutekeleza mpango wa kutambua, kupanga na kupima vipande vya
ardhi na kuweka huduma za jamii kama miundombinu ya barabara na mitaro
ya maji ya mvua ili kuboresha mazingira ya makazi na kuongeza usalama wa
miliki kwa kutoa hatimiliki.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa
Urasimishaji Makazi Holela kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Bibi. Bertha Mlonda wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Akifafanua
Mlonda alisema kuwa mpango huo unatekezwa kwa kushirikiana na
Halmashuri zote za Jiji la Dar es salaam na tayari zoezi limeanza katika
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambapo wananchi wameonyesha
mwitikio mkubwa kwa kuunga mkono juhudi hizo za Serikali.
Akizungumzia
vigezo vinavyofuatwa katika urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela,
Mlonda alibainisha kuwa ni pamoja na eneo husika liwe limetengwa kwa
ajili ya matumizi ya makazi katika Mpango wa Jumla wa Jiji (Master
Plan).
“Mpango
huu ni shirikishi, wananchi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana
na wataalamu kubainisha mahitaji ya huduma za jamii na miundombinu na
siyo makazi holela yote yana sifa ya kurasimishwa. “Alisisitiza Mlonda.
Aidha,
alisema kuwa eneo husika ni lazima liwe na idadi kubwa ya watu wanaoishi
katika eneo hilo ambao hawana uthibitisho wa uhalali wa kumiliki ardhi
hata kama wanalipia ada.
Kigezo
kingine ni kuwepo kwa ongezeko kubwa la ujenzi wa nyumba katika eneo
husika na idadi kubwa ya wakazi ambao wameishi katika eneo hilo kwa
kipindi kirefu.
“Kuna
maeneo mengi ambayo wamiliki wanaendelea kuuza mashamba au viwanja vyao
na ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya makazi na biashara unaendelea kwa
kasi kubwa; ndio maana tumeona ni vyema tukaanza utaratibu huu wa
kurasimisha ili watu wamiliki hayo maeneo kihalali.” Alifafanua Mlonda.
Pia idadi
kubwa ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Asasi za Kijamii
wamehamasika na wako tayari kushiriki katika mipango ya urasimishaji kwa
kuchangia gharama za kupanga, kupima na kumilikisha.
Mlonda
alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na viongozi wao wa Serikali za
Mitaa kutatua migogoro ya mipaka na kutoa ardhi kwa ajili ya barabara
kwani ndio msingi wa ufanisi katika zoezi la urasimishaji makazi.
No comments:
Post a Comment