Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa
Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita
ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na
unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa.
Kulia meza kuu ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye
pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi
huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es
Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Baadhi ya mambo yaliyolengwa katika mkakati huo ni pamoja na udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe, udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari pamoja na kuanza utaratibu wa Mfumo Nukta (point system) kwenye leseni za udereva ambapo dereva akifanya makosa kadhaa atanyang’anywa leseni na kutokuruhusiwa kuendesha gari tena. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment