Monday, August 15, 2016

Mbunge wa CUF akamatwa kwa uchochezi


Mbunge huyo alikamatwa juzi na Jeshi la Polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa sita kwa tuhuma za kufanya mikutano ya hadhara na kutoa lugha za uchochezi za kutomtambua Meya wa Jiji la Tanga, Mustapha Selebosi (CCM).

Taarifa za awali zinasema kuwa, mbunge huyo kabla ya kutiwa mbaroni, alipelekewa barua ya kuhitajika katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul kwa mahojiano zaidi.

Taarifa hizo zinasema kuwa, baada ya mbunge huyo kuitikia wito huo, aliwekwa chini ya ulinzi na kuanza kuhojiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti Chama cha Wananchi (CUF), Mkoa wa Tanga, Rashid Jumbe, alithibitisha mbunge huyo kukamatwa na kusema wakati wa tukio alikuwa na madiwani wa chama hicho.

“Inasemekana alikamatwa na madiwani kwa tuhuma za kutaka kufanya mikutano ya hadhara ya kuwashukuru wananchi kutokana na ushindi walikipa chama chetu.

“Juzi walianza kufanya mikutano hiyo kwenye Kata ya Mwanzange jijini Tanga ambayo ilihudhuriwa na mbunge na jana walifanya mkutano wao kwenye eneo la Madina, Kata ya Msambweni.

“Baada ya kumalizika kwa mikutano hiyo, ndipo asubuhi mbunge huyo alikamatwa na jeshi hilo na kutakiwa yeye na madiwani wasiendelee na mikutano hiyo kwa madai kuwa ni ya kichochezi,” alisema Jumbe.

Naye Kamanda Paul alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi ili azungumzie tukio hilo, alisema alikuwa kwenye kikao.

No comments:

Post a Comment