Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem wakiwa
wamekalia madawati mawili kati ya 50 yaliyotolewa na Kuwait na
kukabidhiwa kwake na balozi huyo jijini Dar es salaam Agosti 17, 2016..
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 12 kutoka mashirika
ya misaada ya Kuwait kwa ajili ya kununulia madawati ili kupunguza
tatizo hilo nchini. Pia amepokea madawati 100 kutoka ubalozi wa Kuwait
na taasisi ya Direct Aid ya nchi hiyo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo (Jumatano, Agosti 17, 2016), Balozi wa
Kuwait nchini Tanzania, Bw. Jasem Al Najem amesema msaada huo ni
michango kutoka mashirika ya misaada ya nchi yake ambayo yanatoa huduma
mbalimbali hapa nchini.
“Tumejipanga
kukamilisha ahadi ya madawati 600, tunaendelea kuwasiliana na wenzetu
wa Kuwait Fund, na mashirika mengine. Kwa sasa tunachangia madawati,
baadaye tutakwenda kwenye ujenzi wa madarasa, hata ikibidi tutaenda
kwenye ujenzi wa shule,” alisema.
Balozi
Najem amesema wanatoa misaada hiyo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais
Dkt. John Magufuli za kutaka wanafunzi wote wakae kwenye madawati.
Akitoa
shukrani mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri Mkuu alimshukuru
Balozi wa Kuwait kwa moyo wao wa kujitolea ikizingatia kuwa ni wiki tatu
tu zilizopita alikwishatoa msaada mwingine wa madawati kwenye shule ya
msingi Chamazi, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Aliyashukuru
pia mashirika ya misaada kupitia Ubalozi huo, ambao wametoa fedha kwa
ajili ya ununuzi wa madawati. Ametoa wito kwa mabalozi wengine, sekta
binafsi na wadau wa maendeleo watoe michango zaidi ili yapatikane
madawati ya kutosha.
No comments:
Post a Comment