Tuesday, August 30, 2016

MAANDAMANO YA UKUTA LABDA YAFANYIKE NDANI KUZUNGUKA KITANDA NJE TUTAPAMBANA VIKALI - DC KASESELA



MKUU wa wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela (pichani) amesema amekwisha  zungumza na makundi  mbali mbali ya  vijana katika wilaya ya  Iringa na  kukubaliana kutoshirikia maandamano ya umoja  wa kupinga  udikteta  Tanzania (UKUTA)  japo anayehitaji   kuandamana  ruksa  ila aandamane ndani ya  nyumba yake  kuzunguka  kitanda na  sio kutoka mitaani.
Akizungumza na vijana  katika  ukumbi wa Highlands mjini hapa wakati wa uzinduzi wa Filam ya  Figisu  ya  Ndoa ,mkuu  huyo  alisema  kuwa  vijana  wanapaswa   kufanya kazi  za  kuwapatia  kipato  na  sio  kutumikishwa  kufanya  maandamano hayo ambayo  kwao hayana faida  yeyote .

"Tumejipanga   kuwashughulikia   wote  watakakaidi agizo  la  serikali kuhusu maandamano ya  UKUTA ......kama  mtu yeyote ana hamu  ya  kufanya maandamano afanye  ndani ya  nyumba  yake   kuzunguka  kitanda  chake na sio  nje mara  baada ya  kumaliza kufanya maandamano ndani kwake anapotoka  nje ni kwa ajili ya  kwenda  kufanya kazi  itakayomuigizia  kipato na sio kwenda  vijiweni ama kwenye  maandamano ya  UKUTA ole  wake mtu  akutwe akiandamana  ama  kupanga kuandamana "alisisitiza Kasesela 

Kuwa  serikali iliyopo madarakani  ni  serikali yenye uchungu na maisha  ya  watanzania na  kuwa  moja katika  ya  mikakati  yake ni kuona kila mtanzania anakuwa na maisha  bora  na  hakuna   njia ya  mkato ya  kuyafikia maisha  bora zaidi ya  kufanya kazi na sio  kutumika  kufanya maandamano ya  kuvutana na  serikali .

Mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema amekwisha pata  taarifa  za  mmoja kati ya viongozi wa Chadema ambaye  ameendelea  kuhamasisha vijana  kufanya maandamano kwenye maeneo  mbali mbali ya  wilaya  hiyo  na  kuwa mipango yote tayari ameipata  hatua  mbali mbali kuchukua hatua  dhidi ya kiongozi  huyo  zinafanyika japo alisema mpango  wao  huo katika wilaya  ya  Iringa hautafanikiwa .

" Wakati  serikali  imezuia  mtu ama   chama  chochote  cha  siasa  kufanya mikusanyiko siku ya Septemba mosi  mwaka  huu  yupo mmoja kati ya  viongozi wa  Chadema ambaye anaendelea  kusambaza ujumbe  kwa  ajili ya kuandaa maandamano  ya  UKUTA .....nasema hakuna  aliyejuu ya  sheria  tutashughulika na uvunjaji  huu wa sheria unaofanywa na kiongozi  huyo"

Aidha  aliwataka  vijana kutokubali  kuingizwa katika matatizo  na kiongozi  mmoja mwenye lengo  baya  dhidi  yao na  badala  yake  kupuuza wito  wake  na  kuendelea na shughuli  zao za  kila  siku .

Kasesela  alisema amepata   kufanya  vikao na makundi  mbali mbali kwa  kuwashirikisha baadhi ya madiwani wa kata  mbali mbali  wakiwemo  wa Chadema na wameapa  kutoshiriki maandamano  hayo .

No comments:

Post a Comment