Tuesday, August 16, 2016

Idris Sultan na Wema Sepetu wazinguana tena

Idris Sultan na Wema Sepetu wamezinguana kwa mara nyingine tena.

Kisa na mkasa ni Wema kuisusia show ya Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo wa Big Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika mwezi uliopita.

Baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake kutompa support kwenye show zake, Idris naye aliamua kuipotezea show ya Usiku wa Vigoma iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo ndipo mambo yalipoharibika. Mashabiki wa Wema wamekasirika baada ya shemeji yao kuikwepa show hiyo na wanamshambulia Instagram.

 Kutokana na kuandamwa, Idris amelazimika kuongea:

"Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?

"Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja.

“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia TusichukulianePoa."

Hata hivyo Wema naye alimpigilia msumari wa moto Idris kwa kupost picha ya wanaume anaowapenda #MCM (Man Crush Monday) na mmoja wao ni Diamond.
Wengine ni Alikiba, Korede Bello, Jamal wa Empire, Cyrill, Trey Songz, Van Vicker na wengine.

No comments:

Post a Comment