Tuesday, August 23, 2016

DMX apata mtoto wa 15


Rapper mkongwe wa muziki wa hiphop DMX Ijumaa iliyopita, alipata mtoto wa 15, wa kiume.  DMX kwa sasa ana miaka 45.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, DMX amempa jina mtoto huyo la Exodus Simmons. Mama wa mtoto huyu ni mpenzi wa muda mrefu wa DMX, Desiree na huyu ni mtoto wake wa kwanza.
DMX kwa sasa yupo studio na Swizz Beatz wanatayarisha ngoma mpya. Wakati mtoto huyo anazaliwa DMX hakuwepo.

No comments:

Post a Comment