Tuesday, August 16, 2016

DC MTATURU AKUBALI OMBI LA WANANCHI LA UHAWILISHAJI ARDHI YA KIJIJI KUWA ARDHI YA KAWAIDA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wanachi wa Kijiji cha Nkuninkhana ili kujua lengo la ombilao la uhawilishaji wa ardhi ya maeneo yao
 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya kwenye mkutano wa hadhara
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturuakizungumza na wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Nkuninkhana ili kujua maendeleo yao katika kujiandaa na mtihani wa darasa la saba
 Chini ya miti kinatafutwa kivuli ili kuleta umakini katika kusikiliza yale yanayozungumza

 Viongozi wa Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Watumishi wa umma, Afisa Tarafa, Mtendaji Kata, Mtendaji wa Kijiji kwa pamoja wakifuatilia maoni ya wananchi
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini ushauri wa kujisomea kwa muda wa ziada wanapokuwa majumbani mwao ili kujikumbusha kwa kile walichofundishwa kutwa nzima
Wananchi wa Kijiji cha Nkuninkhana kwa pamoja wakishiriki mkutano wa hadhara ili kusikia kauli ya Mkuu wa Wilaya kuhusu kukubali ombi lililotumwa ofisinikwake na wananchi wa kijiji hicho la Uhawilishaji wa ardhi
Dc Mtaturu akiwasalimu wakazi wa Kijiji cha Nkuninkhana kwa lugha ya kinyaturu ishara ya kuendeleza utamaduni wa kabila hilo
Wanafunzi wa darasala saba shule ya msingi Nkunikhana wakisikiliza kwa makiniahadi waliyopewa na Dc Mtaturu zawadi ya wanafunzi watakaofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba



Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekubali ombi la wananchi wa kijiji cha Nkuninkhana, Kata ya Puma, Tarafa ya Ihanja ya kutaka uhawilishaji wa ardhi ya Kijiji kuwa ardhi ya kawaida chini ya usimamizi wa Kamishina baada ya kuthibitisha kuwa wanananchi wameshirikishwa kikamilifu.

Amesema kuwa ushiriki wake katika jambo hilo ni kumuandikia barua waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kwamba uhawilishaji wa ardhi yenye Hekta 1327 zilizopo katika Kijiji hicho zitoke kwenye usimamizi wa serikali ya kijiji kwenda kwenye ardhi ya kawaida.

Dc Mtaturu ameridhia ombi hilo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na kusema kuwa kutokana na migogoro iliyojitokeza kwenye mchakato kama huo wa Kijiji cha Nkuninkana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi amewaagiza wakuu wa Wilaya kupokea maombi yote ya uhawilishaji ardhi ili kunusuru kadhia zilizokuwa zinawakumba wananchi.

Mtaturu amewataka wananchi kutambua kuwa maendeleo ni mashindano yanayotaka juhudi na kujituma hivyo amewasihi baadhi ya wananchi kuacha tabia ya kujitangaza kuwa ni masikini ilihali hawashiriki kwa ufasaha shughuli za maendeleo.

Amewataka wananchi kutofanya kazi kwa mazoea kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma juhudi za serikali kama ambavyo wananchi wamerudisha nyuma ujenzi wa maabara na kupelekea kuduma duni za elimu Wilayani Ikungi kwa wanafunzi wanaopenda kusoma masomo ya sayansi.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kufuga kuku kwa tija na mafanikio tofauti na ilivyo sasa wananchi kwa asilimia kubwa wanafuga kuku kwa mazoea huku akisisitiza agizo alilolitoa la kutaka kila kijana alime Heka tatu za kwake binafsi na kila mkulima kulima zao la biashara katika Heka mbili.

Dc Mtaturu pia ameahidi kuwachukulia hatua kila viongozi wote waliochaguliwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi lakini wameshindwa kuyakabili majukumu yao badala yake wamekuwa wapiga debe wa siasa zisizo na tija.

Kijiji cha Nkuninkhana hapo awali katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kilitenga eneo hilo kwa ajili ya upimaji wa viwanja kisheria na pia mpango huu ulisukumwa na kuzuia ujenzi holela ikizingatiwa eneo hilo lipo pembezoni mwa barabara kuu ya Singida kwenda Dodoma, kuipa thamani ardhi hiyo, Kuzuia uuzaji wa ardhi kiholela bila kuzingatia mahitaji ya eneo husika na kusaidia wananchi kupata mikopo katika taasisi za fedha n.k.

Kijiji cha nkuninkhana ni miongoni mwa vijiji vingine vinavyounda Kata ya Puma, kilianzishwa mwaka 1977 huku wananchi wake kwenye kaya 482 na wakazi 2705 asilimia kubwa wakijihusisha na kilimo na Ufugaji.




No comments:

Post a Comment