Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed
Janabi (kulia) akimkaribisha Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan
wakati alipotembelea taasisi hiyo jana.
Balozi wa
Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akisikiliza ripoti ya shughuli za
kitibabu zinazotolewa na taasisi hiyo kutoka kwa Profesa Mohamed Janabi.
Balozi wa
Israel nchini Kenya, Yahel Vilan (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed
Janabi (kulia) wakiingia katika chumba cha upasuaji jana katika taasisi
hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Huduma za Upasuaji JKCI, Dk Bashir Nyangasa akifafanua jambo
kwa balozi huyo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi
maalumu.
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akizungumza na madatari, wauguzi na wataalamu wengine wa taasisi hiyo jana.
Madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wakimsikiliza Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan jana kwenye taasisi hiyo.
Balozi wa
Israel nchini Kenya, Yahel Vilan (kulia) akisaini kitabu cha wageni
kabla ya kupata taarifa fupi ya taasisi hiyo kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed
Janabi.
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akizungumza na madatari, wauguzi na wataalamu wengine wa taasisi hiyo jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza kwenye mkutano huo jana.
Dk Peter Kisenge akimkabidhi zawadi balozi huyo jana.
Wafanyakazi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha pamoja jana.
Na John Stephen
Dar es
Salaam, Tanzania. Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan jana
ameitembela Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kuahidi kutoa mafunzo
kwa wataalamu wa taasisi hiyo.
Balozi
huyo ametembelea chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na
vyumba vya upasuaji pamoja na kuwaona wagonjwa wodini.
“Nimefurahishwa
kusikia kuna madaktari ambao wamesoma Israel na ninapenda kuwaahidi
kuwa Serikali yangu itaendelea kuisaidia tasisi hii, lakini sitatoa
hela,” amesema jana.
Pia
amesema kuwa anafarijika kuona shughuli za kitabibu zinazofanywa na
taasisi hiyo kwa kuwa amekuwa akitaka kwenda kuitembelea lakini hakuwahi
kupata nafasi hivyo amefurahi kupata fursa hiyo.
Wakati
huo huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi
amesema wanakabiliwa na upungufu wa wataalamu sawa na asilimia 50.
“Tunahitaji
wataalamu 278, sasa tuna wataalamu 147 kwa mfano tuna wauguzi 96,
mahitaji halisi ni wauguzi 150,” amesema Profesa Janabi.
Katika
hatua nyingine, Profesa Janabi amesema hospitali hiyo tayari imewafanyia
upasuaji zaidi ya watoto 600 kuanzia mwaka jana hadi sasa.
Profesa
Janabi amesema taasisi hiyo imewekeza zaidi katika kununua vifaa tiba
vya kisasa na kuwawezesha madaktari na wauguzi kupata mafunzo kutoka nje
ya nchi ikiwamo Israel.
Amesema kuwa mpango huo umesaidia wagonjwa wengi kufanyiwa upasuaji ambao umekuwa ukifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.
No comments:
Post a Comment